Monday, September 5, 2016

MAJAMBAZI WAKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM WAKIWA NA SILAHA.

Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limekamata watu watatu wanaoshutumiwa kuwa ni majambazi na kukamata silaha na vifaa vya aina mbalimbali zikiwemo bunduki, risasi, redio call pamoja na sare za polisi katika msako maalumu wa kukamata waharifu.

Akizungumsha na vyombo vya habari kamanda wa polisi mkoa wa Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro amesema baada ya kuwahoji watuhumiwa hao walisema wana nyumba wanaishi eneo la Mbezi chini na kuzikamata silaha hizo kwenye nyumba, ambapo pia ilidaiwa kuwa majambazi hao ni raia wa Kenya.

Sirro amezitaja silaha hizo ni kama SMG 3, bastola 16, shotgun 3 pamoja na risasi zaidi ya 800.

Mbali na silaha hizo pia Sirro amesema pia polisi wamekamata redio call 12, sare za polisi, pingu 45 na darubini 3.


No comments: