Monday, September 5, 2016

MTUHUMIWA MWINGINE ALIYEHUSIKA KWENYE MAUAJI YA DADA WA BILIONEA MSUYA APATIKANA.

Marehemu Aneth Msuya

Idadi ya washtakiwa katika kesi ya mauaji ya Aneth Msuya ambaye alikuwa dada wa Bilionea maarufu mkoani Arusha, Erasto Msuya imeongezeka na kufikia wawili baada ya mwingine kuunganishwa nayo.

Awali Agosti 23, mwaka huu mshitakiwa Miriam Mrita (41) ambaye ni mke wa bilionea huyo alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shtaka la mauaji ya Aneth aliyekuwa wifi yake.

Hata hivyo juma moja baadae mfanyabiashara wa jiji hilo, Revocatus Evarist (40) alipandishwa kizimbani katika mahakama hiyo na kuunganishwa na Miriam kwenye kesi hiyo.

Evarist alipandishwa kizimbani mahakamani hapo ijumaa iliyopita na kusomewa shtaka la mauaji ya Aneth na Wakili wa serikali, Diana Lukondo.


No comments: