Tuesday, October 25, 2016

GARI LILILOIBIWA LIKIWA NA MTOTO LAPATIKANA BAGAMOYO.

Hatimaye gari liloibwa likiwa na mtoto ndani la Ofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Innocent Dallu, limepatikana Bagamoyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Bonventura Mushongi aliwataja waliokamatwa na gari hilo kuwa ni Ezekiel Daudi (25), mfanyabiashara na mkazi wa Moshi aliyekuwa kwenye gari hilo huku aliyekuwa anaendesha Joshua Eliya Adam akitoroka. Daudi analisaida Jeshi la Polisi kuhusu tukio hilo.
Mtego uliowekwa na Jeshi la Polisi katika barabara ya Bagamoyo-Msata, Kata ya Kiwangwa juzi usiku uliwezesha kunaswa kwa wezi pamoja na gari waliloiba.
Watu hao waliiba gari aina ya Toyota Harrier T400DEH mali ya ofisa afya wa JWTZ ambaye alikuwa akifanya kazi katika Hospitali ya Lugalo na kwa sasa amehamishiwa Darfur nchini Sudan ingawa sasa yuko mapumzikoni jijini Dar es Salaam.
Wakati gari linaibwa ndani kulikuwa na watoto wawili, lakini walimshusha mmoja wa kiume Phillip na kuondoka na mwingine wa kike mwenye umri wa miaka mitatu, Lightness Dallu.

No comments: