JAKAYA MRISHO KIKWETE .
Dar es Salaam. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Jakaya Kikwete amependekeza chuo hicho kupewa tuzo ya heshima baada ya kutoa wahitimu walio na mchango katika nyanja mbalimbali nchini, akiwamo Rais John Magufuli na Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa.
Kikwete amesema hayo jana alipokuwa akifungua maadhimisho ya miaka 55, tangu kuanzishwa kwa chuo hicho.
“Chuo hiki kilianza na wanafunzi 14 kikiwa maeneo ya Lumumba ila kwa sasa tunahudumia wanafunzi 24,000 kutoka ndani na nje ya nchi, hii ni hatua kubwa, kimeleta mchango mkubwa sana kwa taifa,” amesema.
No comments:
Post a Comment