Tuesday, January 17, 2017

SOULJA BOY ATOA WIMBO WA KUMTISHIA CHRIS BROWN.

Image result for CHRIS BROWN AND SOULJA BOY
SOULJA BOY NA CHRIS BROWN.
Siku ya jana SOULJA BOY alitoa nyimbo yake mpya inayoitwa ''STOP PLAYING WITH ME'' wimbo ambao ulikuwa ni dongo kwa CHRIS BROWN na Chris alipaniki na kuja juu huku akiukandia wimbo huo na kumwambia Soulja boy aache kuimba kama ndo nyimbo zenyewe ndo hizo.

Chris alitaka kutoa nyimbo siku ya leo lakini amehairisha kwa sababu leo ni kumbukumbu ya MARTIN LUTHER KING na kuamua kuwa mpole siku ya leo.

Unafikiri Chris atatoa nyimbo ya kumjibu Soulja au ataachana na bifu hilo na kuendelea na maisha yake? Drop your comment hapa.

DIAMOND NA ZARI KWENYE JARIDA KUBWA LA AFRIKA KUSINI.


Jarida kubwa na linaloongoza kwa mauzo (PREGNANCY AND BABY GUIDE MAGAZINE) la nchini Afrika ya kusini limempa shavu DIAMOND na mama watoto wake ZARI.


Jarida litatoka wiki ijayo. BIG UP CHIBU.


DIAMOND PLATNUMZ: NAISAPOTI UGANDA KWENYE MASHINDANO YA AFCON KWASABABU NI MASHEMEJI ZANGU KWA ZARI.

Image result for diamond platnumz
DIAMOND & ZARI.
Msanii wa kizazi kipya anayejiita ''SIMBA'' yani DIAMOND PLATNUMZ, jana usiku alifunguka wakati anahojiwa kwenye kipindi cha SPORTS XTRA cha CLOUDS FM.

Diamond alisema anaisapoti Uganda kwa sababu wanaiwakilisha East Africa kwenye michuano hiyo na sababu nyingine ni mashemeji zake kwa ZARI.


Uganda leo usiku wanatupa karata yao ya kwanza kwenye michuano hiyo, wanakipiga vs Ghana majira ya saa 1 usiku kwa saa za Afrika mashariki.



Monday, January 16, 2017

FIFTH HARMONY KUTUMBUIZA KWA MARA YA KWANZA BILA CAMILA CABELLO.

Fifth Harmony, Instagram
FIFTH HARMONY.
Kundi la Fifth Harmony wapo tayari kuwaonyesha mashabiki kuwa wanaweza hata bila ya Camila Cabello ambaye alijitoa mwishoni mwa mwaka jana kwenye kundi hilo.

Kundi hilo litatumbuiza siku ya Jumamosi kwenye 2017 PEOPLE'S CHOICE AWARDS bila ya Camila.

PRIYANKA CHOPRA APATA MAJERAHA WAKATI WA KU-SHOOT SERIES YA QUANTICO.

PRIYANKA CHOPRA.

Priyanka Chopra tweeted, "Thank you for all of your warm thoughts and well wishes. I will be ok, and am looking forward to getting back to work as soon as I can. Much ♥."

Mcheza filamu Priyanka Chopra aliyepata umaarufu kwenye series ya QUANTICO amepata ajari wakati yupo kambini ana-shoot series hiyo.

Alipata majeraha hayo siku ya Alhamisi usiku na kulazwa hospitali. Lakini kwa sasa Priyanka ameruhusiwa kutokana na hali yake kuwa shwari na kuendelea vizuri.

MWANAMIEREKA JIMMY SNUKA AFARIKI DUNIA.

Jimmy Snuka
MAREHEMU, JIMMY SNUKA.
Mwanamiereka wa WWE,Jimmy Snuka maarufu kama 'Superfly' amefariki akiwa na umri wa miaka 73.
Wakili wake amesema mwanamiereka huyo aliaga dunia akiwa katika nyumba ya mkwe wake mjini Florida, akiwa pamoja na familia yake.
Mzaliwa huyo wa Fiji alikuwa wakati mwingi hospitalini kwa shida tofauti ikiwemo ugonjwa wa kiakili wa Dementia, lakini chanzo cha kifo chake bado hakijabainika
Katika taarifa kwenye mtandao wa shirika la WWE imesema imesikitishwa na kifo kilichompata 'mwanzilishi wa kitengo cha high flying' katika ukumbi wamiereka.
Mtoto wake Tamina Snuka, pia nyota wa miereka, aliandika kwenye mtandao wa Twitter, 'Nakupenda babangu' na kuambatisha picha yake na babake kwenye ujumbe wake huo.
Ni chini ya wiki mbili tangu, mashtaka ya mauaji kutupiliwa mbali dhidi yake kuhusiana na kifo cha mpenzi wake mwaka 1983.
Jaji alitoa uamuzi huo baada ya kubaini Jimmy alikuwa na upungufu wa kiakili na hangeweza kuendelea na kesi hiyo ya mauaji ya mpenzi wake Nancy Argentino.
Mashtaka hayo waliwasilishwa mahakamani mwaka 2015.
Alikana madai hayo ya mauaji.
Nyota wa miereka wamekuwa wakituma risala za rambirambi kwa Snuka kwenye mitandao ya kijamii.

Saturday, January 14, 2017

WHATSAPP KUJA NA UWEZO WA KUWAWEZESHA WATUMIAJI KUFUTA UJUMBE KABLA YA KUMFIKIA MUHUSIKA.


WhatsApp-4-840x561

Mtandao maarufu wa kijamii WhatsApp upo katika harakati za kuwawezesha watumiaji wake kufuta ujumbe uliotumwa kabla haujapokewa upande wa pili. 

Kuna wakati unaweza kutuma ujumbe fulani kwa bahati mbaya na kugundua umefanya kosa katika WhatsApp, lakini ukashindwa kuufuta kwa sababu tayari umeshatumwa na kupokewa.
Lakini kwa sasa WhatsApp imekuja na wazo la kurekebisha tukio kama hilo kwenye simu zenye mfumo endeshi wa iOS.

Katika hilo kutakuwa na program katika eneo la ‘Settings’, ambapo utatakiwa kue-‘Edit’ kisha ‘Revoke’ mchakato utakaowezesha kufuta ujumbe huo kwa wakati mara tu unapogundua umekosea.
Hata hivyo, kikubwa ni kuwa utaweza kufanya hivyo kama tu uliomfikia bado hajausoma, ikimaanisha iwapo ameshausoma hutaweza kuufuta.

Lakini hadi sasa WhatsApp hawajatoa taarifa rasmi ya lini uwezo huo utaanza kutumika.