Sunday, August 21, 2016

MFANYABIASHARA AJILIPUA NYUMBANI KWAKE JIJINI MOSHI.

Wakati mfanyabiashara huyo amejilipua

Inawezekana likawa ni tukio baya lililoacha simanzi na majonzi baada ya mfanyabiashara maarufu jijini moshi Romani Shirima (74) kujiua kwa kujilipua kwa petroli nje ya nyumba yake.

Habari kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zinasema mfanyabiashara huyo alijifunika kwa blanketi, kisha kujimwagia petroli kwa kutumia kibiriti kuwasha moto ambao ulimlipua na kusababisha kifo chake.

Ingawa hakuna taarifa ya nini kilichosababisha mfanyabiashara huyo kuchukua uamuzi huo mgumu ulioacha maswali mengi, lakini baadhi walisema ni msongo wa mawazo uliotokana na madeni.

Hili ni tukio la pili kwa mfanyabiashara mkazi wa mkoa wa Kilimanjaro, kwani miaka kadhaa iliyopita, mfanyabiashara anayemiliki hoteli eneo la marangu alijilipua kwa petroli katika gari lake.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 11:25 asubuhi maeneo ya mjohotoni.

Alisema mfanyabiashara huyo ni mmiliki wa shule ya sekondari ya Merinyo iliyopo mjini Moshi na kusema kuwa aliamka asubuhi nyumbani kwake na kujimwagia mafuta hayo na kisha na kujilipua na kibiriti.

Kamanda Mutafungwa alisema chanzo bado hakijafahamika ingawa kuna maneno yanayoongelewa na watu, lakini hawawezi kuyachukua moja kwa moja na kwamba jeshi hilo linachunguza ili kubaini chanzo chake.

Taarifa za tukio hilo la aina yake limekuwa gumzo katika maeneo mbalimbali ya jiji la Moshi na vitongoji vyake.


RAIS WA MAREKANI BARACK OBAMA AKASIRISHWA NA TABIA YA BINTI YAKE MALIA.

Kama inavyotegemewa kwa baba yeyote duniani, tabia ya binti yake Malia imemkasirisha sana Obama.

Hivi karibuni Malia alionekana akivuta bangi katika tamasha kubwa sana.

Kwa mujibu wa tovuti ya Radaronline kitendo hicho kimemsononesha sana Obama anayemaliza muda wake mwaka huu.

Video ilisambaa ikimuonesha Malia akiwa anavuta bangi bila wasiwasi wowote.

Malia alihitimu mwaka huu kwenye shule maalumu ya Sidwell Friends of Washngton DC na anatarajia Kujiunga katika chuo cha Harvard mwaka 2017, chuo ambacho wazazi wake walisoma.


Saturday, August 20, 2016

WATOTO WAINGIZWA KWENYE JESHI SUDANI KUSINI.

Serikali ya Sudani kusini imewaajiri watoto wavulana kama wanajeshi wakati huu inapojiandaa kwa mzozo mpya kwa mujibu wa shirika la Associated press.

Mwanasiasa mmoja mwenye ushawishi anaripotiwa kuongoza shughuli ya kuwaajiri watoto hao, wengine wakitajwa kuwa na umri hadi miaka 12 kutoka kijiji kimoja nchini humo.

Nyaraka zinaonyesha kuwa shughuli za kuwaajiri watoto hao ilifanyika muda mfupi baada ya baraza la usalama la  umoja wa mataifa kuidhinisha azimio wiki moja iliyopita la kutuma wanajeshi 4000 kwenda Sudani kusini, kuwalinda raia baada ya kuzuka mapigano mapya katika mji mkuu Juba mwezi uliopita.

Mapigano hayo yamekuwa kati ya vikosi watiifu kwa rais Salva Kiir na vile vya makamu wake aliyefutwa kazi Riek Macha ambaye tayari amekimbia nchi hiyo.


PICHA YA MVULANA WA SYRIA ILIYOWASIKITISHA WENGI.

Picha ya mvulana mdogo akiwa ameketi kwenye gari la  kubebe wagonjwa Syria, imeweka wazi madhara wanayopitia raia nchini humo.

Mvulana huyo anaonekana akiwa amejaa damu na vumbi baada ya kutelekezwa kwa shambulio la angani mji wa Aleppo.

Picha hiyo ya Omran mwenye umri wa miaka 4, imesambaa sana mtandaoni sawa na ilivyofanya picha ya mwili wa Aylan Kurdi, uliopatikana ufukweni mwa uturuki mwaka jana.

Omran alitolewa kwwnye vifusi baada ya kutelekezwa kwenye shambulio la angani Jumatano katika eneo la Qaterji, kusini mashariki mwa Aleppo.

Watu 290,000 wameuawa na mamilioni wengine kutoroka makwao katika vita vilivyoanza mwaka 2011 nchini humo.


WEMA AKANUSHA KURUDIANA NA DIAMOND.

Ndani ya wiki hii kumetokea vitu vingi kati ya Wema na Idris kugombana, mpaka kupelekea Idris kufuta akaunti yake ya Instagram.

Sasa siku mbili zilizopita kulikuwa na sherehe ya kuzaliwa ya Romeo (Romy Jons) binamu yake Diamond na Wema akahudhuria kwenye sherehe hiyo na kupelekea watu kujua Wema amerudiana na Diamond, kwa sababu alionekana kuwa karibu sana na WCB.

Lakini Wema aliongea kwenye U heard ya Clods FM na kukanusha hizo tetesi kuwa hayupo pamoja na Naseeb.

"Yani watu wakiona naongea na Diamond wanajua tumerudiana, hapana mimi na Naseeb hatuna beef tena nafurahi na nina amani".

Wema alisema hana tatizo na familia ya Diamond na kukanusha kumchukia Tiffa na kukana kumuita Zombie.

"Simchukii Tiffa kwa sababu hajanikosea, yule ni malaika kwa nini nimchukie wakati mimi napenda watoto"

Wema alimalizia kwa kusema kuwa hana shida na Zari kwa sababu ametongozwa na Diamond hana kosa yeye pia ni mwanamke.


BREAKING NEWS: MSANII MKONGWE WA TAARABU BI SHAKILA SAID AFARIKI DUNIA.

Marehemu Bi Shakila amefariki usiku wa jana na sasa mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya jeshi lugalo.

Bi Shakira amewahi kutamba na nyimbo hizi macho yanacheka moyo unalia, hujui alacho kuku pamoja na kifo cha mahaba.

Mwili wa marehemu utapumzishwa leo saa saba mchana.

INALILAH WAINAILLAH RAAJIUN


Thursday, August 18, 2016

MSAFIRI AKANUSHA TETESI ZA YEYE KUSAINI MKATABA NA KAMPUNI YA WANENE.

Muongozaji wa video anayefanya vizuri hapa Bongo kutoka Kwetu Studio director Msafiri Shabani, amefafanua jinsi ya tetesi zilizoenea juu ya kusaini mkataba na kampuni ya Wanene na kuchukua nafasi ya Hanscana.

Msafiri alisema