Wednesday, August 17, 2016

EATV KUTOA TUZO ZA WASANII DISEMBA 10.

Kituo cha Televosheni cha East Africa (EATV) kimeanzisha tuzo za wasanii zitakazofanyika Disemba 10 katika ukumbi wa mlimani city, jijini Dar es salaam.

Mkuu wa masoko wa kituo hicho cha televisheni Mbowe, aliishukuru serikali kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kutoa kibali cha kuendesha zoezi hilo.

Mkuu huyo aliongea
wakati wa uzinduzi wa tuzo hizo katika mkutano was waandishi wa habari.

"Tunatoa shukrani kwa serikali ya Tanzania kutuunga mkono na tutaendelea kufanya kazi na wadau mbalimbali kuboresha tuzo hizi". Alisema Mbowe.

Vodacom ndio wadhamini wakuu wa tuzo hizo. Nandi Mwiyombella mkuu wa masoko wa Vodacom, alisema Vodacom inafurahi kudhamini tukio hili muhimu lenye lengo la  kuwapa motisha wasanii wa kanda ya Afrika Mashariki.

"Moja ya dhamira ya kampuni ya Vodacom ni kuibua na kukuza vipaji ndio maana kampuni imekuwa msitari wa mbele kudhamini michezo na sanaa kwa kuwa inaamini kupitia sekta ya michezo watanzania wengi mbali na kupata burudani inawezesha kuongeza wigo wa ajira. Na kampuni itaendelea kuwezesha wasanii na wanamichezo kama ambavyo hivi sasa inavyodhamini ligi ya soka ya Voda". Alisema Nandi.

No comments: