Wednesday, August 17, 2016

TAYLOR SWIFT ATOA MSAADA WA DOLA MILIONI MOJA KWA WAHANGA WA MAFURIKO HUKO LOUISIANA.

Kwa mara nyingine Taylor Swift anaonyesha jinsi alivyo na moyo wa huruma kwa kusaidia kiasi cha dola milioni moja za kimarekani kwa wahanga wa mafuriko, ambapo nyumba 40,000
ziliharibiwa na watu 11 kupoteza maisha.

"Nawasihi watu ambao wanauwezo wa kusaidia wawasaidie watu hao kwa sababu wanahitaji msaada". Alisema Taylor.

Mafuriko hayo yalitokana na mvua kubwa iliyonyesha tarehe 12, august na kusababisha maafa mengi.

No comments: