Siku mbili zilizopita (jumatatu) Wema Sepetu alituma picha za wasanii kwenye akaunti yake ya instagram wakiwemo Jamal wa kwenye movie ya empire, Trey songz, Korede bello, Cyril kamikaze, Alikiba na Diamond na kuweka caption ya (MCM).
Mashabiki walikuja juu
na kuanza kusema kwa nini Wema hakumuweka Idris kwenye hiyo picha na kwenda mbali zaidi kusema kwa sababu Idris huwa anatuma picha nyingi za wadada.
na kuanza kusema kwa nini Wema hakumuweka Idris kwenye hiyo picha na kwenda mbali zaidi kusema kwa sababu Idris huwa anatuma picha nyingi za wadada.
Baada ya mda Idris aliwajibu kwa kutuma ujumbe mrefu uliowataka wafuasi wake wasimuite shemeji kwa sababu wanamkosesha madili na jina la Idris sasa ni brand kubwa.
Wema kajibu mapigo na kusema yupo kikazi zaidi kwa sasa, hana mda wa kugombana na watoto.
Sasa Idris yamefika maji ya shingo na kuamua kufuta kabisa akaunti yake ya instagram kama alivyofanya Justine Bieber hapo juzi au Elizabeth Michael (Lulu) enzi zile alizoshambuliwaga na mashabiki.
No comments:
Post a Comment