Wednesday, August 17, 2016

KANISA LA P.O.G LAMTAKA MRISHO MPOTO KUVAA VIATU.

Muumini wa kanisa la P.O.G ambaye aligoma kutaja sehemu kanisa linapatikana, ameongea leo kupitia U heard ya Clouda FM kwamba, kanisa lao linamuomba Mrisho Mpoto (mjomba) kuvaa viatu kwa sababu anazuia
baraka za watu.

Muumini huyo alifunguka na kusema kwamba Mungu hapendezwi na kitendo hicho cha Mrisho kutovaa viatu.

Mjomba alipopigiwa simu na kuambiwa hilo jambo alishangaa na kutaka kujua mahali ambapo hilo kanisa lipo ili aanze kwenda kusali.

Mjomba alisema "kutembea bila viatu ni Afya na tiba, karne hizo wazee wetu walikuwa wanatembea peku bila viatu. Kutembea kwangu bila viatu haihusiani na kuzuia riziki za watu".

"Nitaanza kuvaa viatu ili nisije nikawa nazuia baraka za hilo kanisa". Alimaliza kwa kusema hivyo.

No comments: