Wednesday, October 26, 2016

MAJALIWA AWAHAKIKISHIA MIKOPO WANAFUNZI WA VYUO VYA ELIMU YA JUU.



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hadi kufikia kesho, asilimia 90 ya wanafunzi watakuwa wameshapata fedha zao za mkopo wa elimu ya juu.
Majaliwa alisema hayo jana wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 55 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
 “Serikali haitavumilia tena ucheleweshwaji wa makusudi wa malipo ya fedha za mikopo ya chuo. Kama kuna tatizo, taarifa zitolewe haraka ili kuzuia migogoro kati ya wanafunzi na Serikali yao,” alisema.

No comments: