Katika milima ya jimbo la Sichuan kusini magharibi mwa China, kundi la watoto ambalo lilikuwa likishuka mita 800 kwenye mlima ili kufika shule huku wakitumia njia za asili ambazo ni ngazi za miti ambayo ni hatari sasa wanajengewa ngazi za chuma.
Ngazi hiyo ya chuma inayojengwa na wanakijiji itakuwa na mabomba 1,500 ya chuma na inatarajiwa kukamilika mwezi November mwaka huu, ujenzi wa ngazi hizo zenye gharama ya dola za marekani 150,000 ambazo ni karibu Tsh za kitanzania milioni 327, ilianza kujengwa na wanakijiji mwezi August mwaka huu.
Ngazi hiyo inatarajiwa kuwa na muundo imara zaidi pia inatarajiwa itakuwa yenye usalama zaidi kwa hata wanakijiji wa kijiji hicho ambao watakuwa wanaitumia kupanda na kushuka kila wiki kununua bidhaa mbalimbali na kufanya biashara zao katika soko ambalo liko mbali na wanakoishi. Siku za nyuma wanakijiji walikuwa wakitumia miti ya mizabibu ambayo ilikuwa mibovu.
No comments:
Post a Comment