Mhudumu wa Baa ya Golden Brigde iliyopo Kawe, Halima Kamalu amesema baada ya saa tatu ndipo alipotambua kwamba kuna gari na mtoto ameibwa.
Kamalu alikuwa akizungumzia tukio la kuibwa gari la Ofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Innocent Dallu, ambalo ndani walikuwamo wanawe wawili.
Alisema yeye ndiye aliyempokea mteja aliyefika kupata kinywaji akiwa na mtoto, ambaye aliagiza soda mbili na kulipa Sh5,000. Alisema mteja huyo alionja kidogo kinywaji chake kisha aliomba kuelekezwa kilipo kibanda cha kutolea fedha na hakurejea.
Kamalu alisema baada ya saa tatu ndipo akiwa polisi alijua kwamba mtoto huyo alikuwa ameibwa pamoja na gari la baba yake Jumapili iliyopita. Alisema alimpenda mtoto huyo baada tu ya kumwona na kwa muda aliokaa naye alimzoea.
No comments:
Post a Comment