Thursday, October 13, 2016

MENEJA WA ALIKIBA AJIBU TUHUMA ZILIZOTOKEA MOMBASA KUHUSU ALIKIBA.

                                                     MENEJA WA ALIKIBA.
Aidan Charlie ambaye ni meneja msaidizi kutoka kwenye Menejimenti ya mwimbaji staa wa bongofleva Alikiba ameongea kuhusu tuhuma mbalimbali zilizotolewa dhidi ya Alikibakutokana na show ya Mombasa iliyofanyika weekend iliyopita na zifuatazo ni kauli zake.
Sio kweli kwamba Alikiba alisema yeye ni msanii mkubwa Afrika Mashariki hivyo Wizkid ndio alitakiwa kupanda stejini kabla yake, alietoa hizo habari kadanganya.
Kilichotokea ni kwamba kiujumla Waandaaji hawakuwa wamejipanga vyema, show ilitakiwa kuanza saa nane mchana lakini wakaipeleka mbele mpaka saa tatu usiku.
Ishu ilikua wakati Chris Brown alipofika kuliangalia jukwaa na kuzoea mazingira ilibidi seti yote ya Alikiba iliyopangwa jukwaani iondolewe pamoja na watu wa Ali, hiyo ikafanya Alikiba achelewe kufanya rehearsal ambapo alimaliza saa mbili usiku na kurudi hotelini kwenda kujiandaa na show.
Tumerudi tu hotelini tunapigiwa simu kuambiwa mnatakiwa kupanda kwenye stage ikabidi Alikiba arudi uwanjani lakini muda ulikua umeyoyoma na Chris Brown alitakiwa kutumbuiza mapema ili awahi Airport.
Hakuna kutunishiana misuli kokote kati ya Wizkid na Alikiba, wawili hawa wako vizuri na walikua wanaongea backstage na Wizkid alimwambia Ali haondoki uwanjani mpaka aone show yake.

No comments: