Taarifa zinasema wasichana hao kwa sasa wamo mikononi mwa maafisa wa usalama katika mji wa Maiduguri, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Haijabainika iwapo wasichana hao walikomombolewa na wanajeshi au waliachiliwa huru na wanamgambo hao.
Jeshi la Nigeria kwa muda limekuwa likiendesha operesheni kubwa ya kijeshi katika msitu wa Sambisa, ngome ya Boko Haram.
Wapiganaji wa kundi hilo waliteka wasichana takriban 250 waliokuwa wakilala kwenye mabweni shuleni Aprili mwaka 2014.
Kisa hicho kilishutumiwa vikali na jamii ya kimataifa.
Tangu wakati huo, ni msichana mmoja pekee aliyekuwa ameokolewa.
Kundi la kujihami la wanakijiji lilimpata Amina Ali Nkeki mwezi Mei akiwa na mumewe, ambaye anatuhumiwa kuwa mwanachama wa Boko Haram, pamoja na mtoto wake.
No comments:
Post a Comment