Akina dada walioshiriki katika mashindano ya urembo kwa watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi ama Albinos jijini Nairobi, Kenya. Tarehe 21 Oktoba 2016.
Malkia mpya! Louise Lihanda, aliyeshinda taji la urembo kwa akina dada atembea jukwani akiwa amevalia vazi la kupendeza lililotengenezwa kwa kutumia puto. Loiuse ambaye ni mwanafunzi, amekuwa mwanamke wa kwanza kushinda taji hilo, katika mashindano yaliyofanyika jijini Nairobi, Kenya tarehe 21 Oktoba 2016.
Wanaume walioshiriki katika mashindano hayo wasimama tisti jukwaani. walishiriki katika mashindano ya urembo kwa watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi ama Albinos jijini Nairobi, Kenya. Tarehe 21 Oktoba 2016.
Mfalme! Jairus Ongetta, ambaye amekabidhiwa taji ya uanamitindo bora kwa wanaume akiwa jukwaani na mavazi ya kupendeza.
Majaji walikuwa macho! Waliongozwa na mwanamitindo wa kimataifa Deliah Ipupa (katikati) tarehe 21Oktoba 2016.
No comments:
Post a Comment