Monday, October 24, 2016

VIJANA MAARUFU WENYE USHAWISHI ZAIDI 2016.

Malala Yousafzai, Jaden Smith, Kylie Jenner, mabinti wa Obama na Chloe Grace Moretz wote kwa mara nyengine wamejumuishwa katika orodha ya vijana walio na ushawishi zaidi mwaka huu katika jarida la Times magazine.
Inatazama athari walio nayo vijana katika vyombo vya habari na katika mitandao.
Orodha hiyo inajumuisha pia waigizaji kutoka vipindi kama Stranger Things, Game of Thrones na Hunger Games.
Ni nyota kutoka sanaa ya musiki, mchezo uanamitindo, sayansi , biashra na siasa.
Malala Yousafzai alipigwa risasi na Taliban mnamo 2012.
Malala Yousafzai
Tangu hapo amekuwa kijana mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kushinda tuzo ya Nobel ya amani na kupata kimondo kutajwa kwa jina lake, na kuna taaifa kwamba huenda kukatengenezwa filamu kuhadithia maisha yake.
Akiwa na umri wa miaka 19, Malal amejumuishwa katika orodha hiyo ya vijana wenye ushawishi tangu mwaka 2013 na bado anatetea haki za wasichana kusoma kote duniani.

Mamayao anapendwa kote duniani na baba yao ni rais wa kwanza mweusi Marekani.

Malia na Sasha Obama
Kwahivyo hakuna shinikizo kubwa kwa Sasha na Malia Obama?
Ni vizuri kuona kuwa wanafuata nyayo za wazazi wao, huku Sasha akishirikiana na mamake kuhimiza wanawake wanaelimika Liberia na Mali naye Malia akitarajiwa hivi karibuni kujiunga na chuo kikuu cha Harvard.
Awali wakitazamwa kwa sifa ya watu wawili na dadake Kendall, Kylie Jennermwaka huu amepata sifa peke yake.
Kylie Jenner
Wakati Kendall na Kylie wote wakitokea mara tatu katika orodha hiyo ya vijana walio na ushawishi tangu 2013 - mara moja kila mtu kivyake na mara mbili wakiwa pamoja maarufu "iconic duo," Kendall hakujumuishwa mwaka huu kwasababu ametimiza miaka 20!
Kylie anepeperusha sifa ya jina la familia Jenner kwa kuorodheshwa kwa mara ya nne sasa.
Luka Sabbat na Jaden Smith wanawakilisha wanamitindo wanaume wanaosifika.
Luka Sabbat
Katika mtandao wake wa Instagram anajiita mwanamitindo, mjasiriamali bingwa wa mitindo, na ukampata Tom Ford kukutumia suti , hapana shaka kuhusu sifa anazojipa.
Na Jaden hakuachwa nyuma katika suala la kuwana mtindo wake wa mavazi katika siku za nyuma ikiwemo kuonyesha mitindo ya mavazi ya wanawake ya Louis Vuitton.
Huenda unadhani humjui Maddie Ziegler, lakini ukiiona sura yake utamtambua.
Maddie Ziegler
Anasifika kama mchezaji densi katika kanda ya musiki y ya muimbaji maarufu Sia 'Chandelier na The Greatest', na huambatana na mwanamuziki huyo asiyejulikana sura katika tamasha kuonyesha mfano wake.
Maddie alijumuishwa pia katika orodha ya mwaka 2015 na akiwana miaka 14 tu ndiye kijana zaidi kutambuliwa mwaka huu.

Na orodha haiwezi kukamilika mwaka huu pasi kuwataja wanamichezo nyota.

Simone Biles

Simone Biles na Laurie Hernandez katika mchezo wa gymnastics wamejumuishwa pamoja na waogeleaji Katie Ledecky na mkimbiza wa Syria Yusra Mardini waliong'ara katika mashindnao ya mwaka huu ya Olimpiki.

No comments: