Monday, October 24, 2016

WASANII WA BONGO WAAMBULIA PATUPU KWENYE TUZO ZA MTV MAMA.

Tuzo za MTV nchini Afrika Kusini

Wawakilishi wa Tanzania katika tuzo za wanamuziki bora zinazoandaliwa na MTV Africa Music Awards 2016 (MAMA hawakufanikiwa kutwaa tuzo yoyote japokuwa waliweza kushiriki katika vipengele tofauti.
Tuzo hizo zilizotolewa Johannesburg, Afrika Kusini kuamkia jumapili, dalili zilionekana mapema kuwa mbaya kwani Vanessa Mdee aliyekuwa anawania tuzo ya msanii bora wa kike alishindwa baada ya Yemi Alade (Nigeria) kutangazwa mshindi.
Diamond Platinumz aliyekuwa anashindania tuzo ya msanii bora wa mwaka akipambana vikali na Black Coffee, Sauti Sol, Wizkid na Yemi Alade alishuhudia tuzo hiyo akikabidhiwa Wizkid.
Wimbo "Unconditionally Bae" ulioimbwa na Sauti Sol akishirikiana na Alikiba, ambao ulikuwa kwenye kipengele cha wimbo bora wa kushirikishwa haukupata tuzo.
Wimbo huo pia uliambulia patupu katika kipengele cha wimbo bora wa mwaka.
Hata hivyo, Yamoto Band iliyoshiriki katika tuzo hizo katika kipengele cha 'Chaguo la Wasilikizaji' haikufanikiwa kutwaa tuzo hiyo.
Vilevile msanii mwingine kutoka Tanzania aliyeshiriki tuzo hizo maarufu barani Afrika na kushindwa kufurukuta katika medani hiyo ya kimataifa ni Raymond.

No comments: