Wednesday, November 2, 2016

MSHINDI WA MAISHA PLUS ATATUMIA FEDHA ALIZOSHINDA KUSOMEA FILAMU NA KUSAIDIA WATOTO YATIMA NCHINI KENYA.

Olive Kiarie

Mshindi wa Shindano la Maisha Plus msimu wa tano kutoka nchini Kenya, Olive  Kiarie, amesema atatumia fedha alizoshinda kujifunza taaluma ya uandaaji wa filamu.
Akizungumza jana, Olive alisema mbali na kutumia fedha hizo kujifunza filamu, nyingine atazipeleka katika kituo cha kulelea watoto yatima nchini Kenya.
Olive alisema anashukuru kuibuka na ushindi, hivyo ni vema akarudisha shukrani kwa wale waliofanikisha mafaniko yake.
“Nashukuru, kuwa mshindi ni kitu kikubwa, hivyo nimekuja kutoa cheti, kuonyesha jinsi gani nimethamini mchango ulioonyeshwa na gazeti hili.
“Nilipanga kutoa fungu la 10 la fedha nitakazoshinda kwa watoto yatima nyumbani kwetu, hilo lazima nilitimize,” alisema Olive.
Olive alieleza kuwa Tanzania ni nchi yenye watu wakarimu wenye upendo, kupitia shindano hilo ameweza kujifunza mambo mengi.

No comments: