Thursday, October 13, 2016

TUHUMA ZA TRUMP KURUBUNI WANAWAKE BADO ZAZIDI KUPAMBA MOTO.

Jessica Leeds
Wanawake wawili wameambia gazeti la New York Times kwamba mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump aliwashika kimapenzi bila idhini yao.
Mwanamke mmoja amesema mgombea huyo alimshika matiti na kujaribu kuingia mkono wake chini ya sketi yake wakiwa kwenye ndege miongo mitatu iliyopita.
Wa pili anasema Bw Trump alimpiga busu bila yeye kutaka katika jumba la Trump Towers mwaka 2005.
Maafisa wa kampeni wa Trump wamesema "makala hii yote ni hadithi ya kubuni".
Gazeti la New York Times limeanzisha kampeni "ya uongo, na iliyoratibiwa kumharibia jina kabisa", taarifa ya maafisa wa Trump imesema.
Jessica Leeds, 74, kutoka Manhattan, ameambia gazeti hilo kwamba alikuwa ameketi karibu na Bw Trump sehemu ya abiria wa hadhi ya juu kwenye ndege wakielekea New York pale alipoinua sehemu ya kupumzishia mkono kitini na akaanza kumshika.
Mwanamke huyo alikuwa na umri wa miaka 38 wakati huo.
"Alikuwa kama pweza .... mikono yake ilinishika kila pahali," anasema. "Ulikuwa ni unyanyasaji."
Rachel Crooks alikuwa mpokezi wa wageni katika kampuni ya kuuza ardhi ya nyumba katika jumba la Trump Tower, wakati huo akiwa na miaka 22.
Trump Tower in Manhattan
Anasema alipigwa busu la lazima na Bw Trump nje ya lifti ya jengo hilo.
"Ilikuwa vibaya sana," Bi Crooks ameambia New York Times.
"Niliudhika sana kwamba alidhani nilikuwa sina maana kiasi kwamba angefanya hivyo (bila hiari yangu)."
Wawili hao hata hivyo hawakuripoti visa hivyo kwa maafisa wa serikali.

Hata hivyo, wanasema waliwaambia marafiki na jamaa zao yaliyojiri.
Bi Leeds anasema alikasirika sana na alitatizika kimawazo baada ya Bw Trump kumgusa.
Anasema mara moja aliondoka eneo la abiria wa hadhi na kwenda kuketi eneo la abiria wa kawaida.
Maafisa wa kampeni wa Clinton wamesema simulizi hizo za kuogofya kwenye New York Times zinatilia mkazo "kila kitu ambacho tunajua kuhusu jinsi Donald Trump huwachukulia wanawake".

'Kumshika makalio'

Hayo yakijiri, Mindy McGillivray naye ameambia gazeti la Palm Beach Post kwamba akiwa na miaka 23 , Bw Trump alimshika makalio katika kilabu chake cha Mar-a-Lago club jimbo la Florida mwaka 2003.
Anasema alikuwa amesimama karibu na mchumba wake wa wakati huo Melania Knauss.
Bi McGillivray, ambaye kwa sasa ana miaka 36, anasema hakuripoti kisa hicho kwa polisi.
Lakini mwenzake, mpiga picha Ken Davidoff, aliambia gazeti hilo kwamba mwanamke huyo alimwita kando siku hiyo na kumwambia: "Donald amenishika makalio sasa hivi".
Maafisa wa Trump wanasema madai ya Bi McGillivray hayana ukweli wowote.
Wanawake wote watatu wamesema wanaunga mkono Bi Clinton.
Ijumaa wiki jana, video iliyopigwa mwaka 2005 ilitokea na kumuonyesha Bw Trump akinena maneno ya kuwadhalilisha wanawake na kuongea kuhusu kuwapapasa wanawake.
Aliomba radhi kuhusu matamshi hayo, lakini akasema yalikuwa mazungumzo ya mzaha faraghani.
Viongozi wengi wakuu wa Republican, akiwemo Spika Paul Ryan, wameshutumu matamshi hayo. Bw Ryan alisema hatamtetea tena Bw Trump.

WASICHANA 21 WA CHIBOK WAACHILIWA HURU NIGERIA

Afisa wa cheo cha juu serikalini ameiambia BBC kwamba wasichana 21 waliokuwa miongoni mwa wasichana wa shule waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram eneo la Chibok sasa wako huru.
Taarifa zinasema wasichana hao kwa sasa wamo mikononi mwa maafisa wa usalama katika mji wa Maiduguri, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Haijabainika iwapo wasichana hao walikomombolewa na wanajeshi au waliachiliwa huru na wanamgambo hao.
Jeshi la Nigeria kwa muda limekuwa likiendesha operesheni kubwa ya kijeshi katika msitu wa Sambisa, ngome ya Boko Haram.
Wapiganaji wa kundi hilo waliteka wasichana takriban 250 waliokuwa wakilala kwenye mabweni shuleni Aprili mwaka 2014.
Kisa hicho kilishutumiwa vikali na jamii ya kimataifa.
Tangu wakati huo, ni msichana mmoja pekee aliyekuwa ameokolewa.
Kundi la kujihami la wanakijiji lilimpata Amina Ali Nkeki mwezi Mei akiwa na mumewe, ambaye anatuhumiwa kuwa mwanachama wa Boko Haram, pamoja na mtoto wake.
Wasichana 250 walitekwa Aprili 2014

WACHINA WAKAMATWA MTWARA WAKIBADILISHA EXPIRE DATE.

Watu watano wakiwemo raia wawili wa China na Watanzania watatu wamekamatwa Mtwara kwa kutuhumiwa kubadili tarehe zilizokwisha muda wa matumizi kwenye dawa za kilimo (expire date) ili dawa hizo ziingizwe tena sokoni na kuonekana bado zinafaa kwa matumizi.
Inadaiwa watuhumiwa hawa wamefanikiwa kubadilisha dawa hizo kwenye mabox zaidi ya mia sita ( 600) na kuzifanya zionekane mpya ambapo Kamanda wa Polisi Mtwara amesema Watuhumiwa hao walikamatiwa Nangwanda.
Makachero wa Polisi baada ya kupewa taarifa waliwahi kwenye eneo la tukio na kukuta watu wanne wakikwangua chupa kuondoa nembo iliyoonyesha dawa hiyo ilitengenezwa tarehe 28 February 2013 na muda wake wa matumizi umekwisha tarehe 27 February 2016.
Nembo mpya feki waliyoitengeneza Wachina hawa inasomeka dawa imetengenezwa tarehe 20 February 2016 na inamaliza muda wa matumizi tarehe 19 February 2019

RAIS MAGUFULI ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA YA MAREHEMU MASABURI.

                                                  MAREHEMU DIDAS MASABURI.
Rais John Magufuli ameitumia salamu za rambirambi familia ya Meya Mstaafu wa Jiji la Dar es Salaam Dkt. Didas Masaburi aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Taarifa ya Ikulu jijini Dar es Salaam imesema katika salamu hizo Rais Magufuli amesema amepokea taarifa ya kifo cha Dkt. Masaburi kwa mshituko na masikitiko makubwa na kwamba anaungana na familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha huzuni ya kuondokewa na mpendwa wao.

"Poleni sana familia ya Dkt. Didas Masaburi, najua huu ni wakati mgumu sana kwenu, lakini niwahakikishie kuwa sote tumeguswa sana na msiba huu kwa kuwa tumempoteza mtu muhimu, msomi mzuri, kiongozi aliyelitumikia Taifa kwa moyo wake wote na aliyesimamia kile alichokiamini" amesema Rais Magufuli katika salamu hizo.

Aidha, Magufuli amewapa pole wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao wamempoteza Mwana CCM mwenzao pamoja na Viongozi na watumishi wa Jiji la Dar es Salaam ambao walifanya nae kazi alipokuwa Meya wa Jiji.

Amemuombea kwa Mwenyezi Mungu ampumzishe mahali pema peponi.

"Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Amina" amemalizia Rais Magufuli.

MOI YAFANYA UPASUAJI MWINGINE MKUBWA

                                                      DK. OTHMAN KILOLOMA.
TAASISI ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa mara ya kwanza imefanya upasuaji mkubwa kwa mafanikio wa kunyoosha mfupa wa mgongo wa mtoto wa miaka 13 uliokuwa umepinda (kibiongo).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dk Othman Kiloloma amesema jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akielezea upasuaji huo uliofanyika kwa saa tano.

Dk Kiloloma amewaeleza waandishi wa habari kuwa, upasuaji huo umefanyika kwa kutumia teknolojia ijulikanayo kama ‘posterior instrumentation and fusion’ ambayo inahusisha uwekaji wa vyuma maalumu kwenye mfupa wa mgongo katika sehemu ya juu na chini ya mfupa wa mgongo na kuufanya unyooke kama inavyotakiwa.

“Taasisi ya MOI imefanikiwa kufanya upasuaji huo kwa kupitia madaktari bingwa walioko kwenye mafunzo ya ubobezi wa juu katika upasuaji wa mifupa na mgongo kwa watoto kwa kushirikiana na madaktari bingwa kutoka Marekani,” alisema Dk Kiloloma.

Alisema uanzishwaji wa upasuaji huo umetokana na kuanzisha kwa ushirikiano wa kimafunzo kati ya Taasisi ya MOI na Chuo cha Madaktari Bingwa wa Upasuaji cha Afrika Mashariki, Kati na Kusini (COSECSA) na madaktari bingwa kutoka Marekani.

Mkurugenzi huyo alisema uanzishwaji wa upasuaji huo wa kunyoosha migongo ya watoto iliyopinda, unatarajiwa kuisaidia serikali kupunguza rufaa za kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi ambazo ni za gharama kubwa.

“Watoto hao waliokuwa wanaenda India na sehemu nyingine, iligharimu dola 60,” alisema.

MAGUFULI ATUMBUA JIPU LINGINE.


Hatua ya Rais John Magufuli kuzuia viongozi waandamizi wa mikoa na wilaya kuhudhuria kilele cha Mbio za Mwenge mkoani Simiyu, imeokoa Sh1.2 bilioni ambazo zingetumika kulipia posho na usafiri.

Wakuu wa mikoa 30, wa wilaya 161, makatibu tawala wa mikoa na wilaya, wakurugenzi, wenyeviti wa halmashauri na mameya, wasaidizi wa wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, waratibu wa Mwenge wa wilaya na mikoa pamoja na madereva wa viongozi wote hao wangehudhuria sherehe hizo na wangeigharimu Serikali kiasi hicho cha fedha.

Kwa makadirio, wakuu wa mikoa 30 kila mmoja angelipwa posho ya kila siku Sh120,000 kwa siku saba, msaidizi wake Sh80,000 kwa siku na dereva Sh50,000. Katibu tawala angelipwa Sh120,000 kwa siku na dereva wake Sh50,000 wote kwa siku hizo saba.

Wakuu wa wilaya 161 wangelipwa posho ya Sh120,000 kwa siku kwa muda huo na madereva wao Sh50,000.

Katika msafara huo wangekuwapo makatibu tawala wilaya 161 ambao nao wangelipwa posho ya Sh120,000 na madereva wao Sh50,000 kila siku.

Wakurugenzi wa halmashauri 161, wenyeviti na mameya wangelipwa Sh120,000 kwa siku. Madereva wao kila mmoja angepokea posho ya Sh50,000 kila siku kwa muda wa siku saba.
Wengine ambao wangehudhuria sherehe hizo ni waratibu wa Mbio za Mwenge wa mikoa na wilaya ambao walitarajiwa kulipwa posho ya Sh80,000 kila mmoja.


Tofauti na posho hizo, waratibu hao pia wangelipwa nauli za kwenda na kurudi kutoka katika maeneo yao ya kazi na viongozi wengine wa juu wangepewa posho za kununulia mafuta.

MENEJA WA ALIKIBA AJIBU TUHUMA ZILIZOTOKEA MOMBASA KUHUSU ALIKIBA.

                                                     MENEJA WA ALIKIBA.
Aidan Charlie ambaye ni meneja msaidizi kutoka kwenye Menejimenti ya mwimbaji staa wa bongofleva Alikiba ameongea kuhusu tuhuma mbalimbali zilizotolewa dhidi ya Alikibakutokana na show ya Mombasa iliyofanyika weekend iliyopita na zifuatazo ni kauli zake.
Sio kweli kwamba Alikiba alisema yeye ni msanii mkubwa Afrika Mashariki hivyo Wizkid ndio alitakiwa kupanda stejini kabla yake, alietoa hizo habari kadanganya.
Kilichotokea ni kwamba kiujumla Waandaaji hawakuwa wamejipanga vyema, show ilitakiwa kuanza saa nane mchana lakini wakaipeleka mbele mpaka saa tatu usiku.
Ishu ilikua wakati Chris Brown alipofika kuliangalia jukwaa na kuzoea mazingira ilibidi seti yote ya Alikiba iliyopangwa jukwaani iondolewe pamoja na watu wa Ali, hiyo ikafanya Alikiba achelewe kufanya rehearsal ambapo alimaliza saa mbili usiku na kurudi hotelini kwenda kujiandaa na show.
Tumerudi tu hotelini tunapigiwa simu kuambiwa mnatakiwa kupanda kwenye stage ikabidi Alikiba arudi uwanjani lakini muda ulikua umeyoyoma na Chris Brown alitakiwa kutumbuiza mapema ili awahi Airport.
Hakuna kutunishiana misuli kokote kati ya Wizkid na Alikiba, wawili hawa wako vizuri na walikua wanaongea backstage na Wizkid alimwambia Ali haondoki uwanjani mpaka aone show yake.