Masaa machache yaliyopita, msanii wa filamu Wema Abraham Sepetu aleta gumzo kwenye mtandao wa Instagram baada ya ku-post picha ya mastaa mbalimbali wakiwemo Jamal wa kwenye movie ya empire, Alikiba, Cyril Kamikaze, Diamond platnumz, Trey songz, Korede bello na wengine kama picha inavyoonesha hapo juu.
Mashabiki wamjia juu baada ya kutokumuweka anayesemekana ni mpenzi wake Idris Sultan.
Wengine wadai kuwa Wema na Idris wamegombana so Wema kapanick na kuamua kuwa-post hao mastaa na kuweka caption ya #MCM.
Mpaka sasa Wema hajaeleza sababu ya yeye kutomuweka Idris kwenye hiyo picha. Bado tunaendelea kutafuta undani wa hiyo habari.
Usiache kupitia burudaninaangie.blogspot.com kwa updates zote
Monday, August 15, 2016
WEMA SEPETU AZUA UTATA INSTAGRAM
MASANJA HATIMAYE AFUNGA NDOA.
Mchekeshaji maarufu wa kundi la Ze comedy show Masanja mkandamizaji afunga ndoa jumapili ya jana tarehe 14 August. Wiki kadhaa zilizopita Masanja alimvalisha Pete mke wake huyo na hatimaye jana afunga pingu za maisha.
Wasanii wengi wakihudhuria hiyo sherehe wakiwemo Ze comedy, Lulu Michael, Dr. Cheni, Mbasha na viongozi mbalimbali.
NAY WA MITEGO AMALIZANA NA BASATA.
Kama utakuwa unakumbuka 27, 7, 2016 Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) lilitoa tamko la kumfungia msanii wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego kutojihusisha na kazi ya sanaa kwa muda usiojulikana
Sasa leo August 15, 2016 baraza hilo limetoa tamko rasmi la kumfungulia msanii huyo kufanya kazi ya muziki huku akiwa kwenye uangalizi maalum sehemu ya kuhakikisha anaendesha shughuli za sanaa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu na kuzingatia maadlili katika kazi zake.
Kwa mujibu wa Katibu mkuu wa BASATA Godfrey L. Mngereza aliyaongea haya>>>>Itakumbukwa kwamba mnamo tarehe 27/7/2016 Baraza lilimfungia Msanii Nay wa Mitego kwa kipindi kisichojulikana na kumtaka kutekeleza maagizo yafuatayo:
1.Kuhakikisha amesajiliwa na kuwa na kibali cha kuendesha shughuli za Sanaa
2.Kulipa faini ya Shilingi milioni moja (1,000,000/-)
3.Kuomba radhi watanzania kupitia mkutano wa waandishi wa habari na kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii
4.Kuufanyia marekebisho wimbo wa ‘Pale Kati’ ili ubebe maudhui yenye maadili
‘Msanii huyo ametekeleza adhabu zote zilizotajwa hapo juu, hata hivyo pamoja na kuleta marekebisho mara mbili ya wimbo wa ‘Pale Kati’ Baraza bado halijaridhishwa na marekesho hayo hivyo linaendelea kuufungia wimbo huo hadi hapo litakapojiridhisha umekidhi vigezo vya kimaadili‘- Godfrey Mngereza
BASATA limetoa agizo kwa msanii huyo kuendelea kuufanyia marekebisho wimbo wake huo kama bado atakuwa anauhitaji.
Source millardayo.com
DIRECTOR HANSCANA ATANGAZA KUACHANA NA WANENE ENTERTAINMENT
Director maarufu hapa nchini Hascana, ametangaza rasmi kuachana na Wanene na kuanza maisha yake mapya. Hanscana alisema hajagombana na uongozi wa wanene entertainment bali ameamua kuondoka ili aanzishe maisha yake mwenyewe, kwasababu amekuwa sasa (23).
Director huyo ameondoka na crew yake nzima ya videos department tangu tarehe 4 mwezi huu wa nane, kwasababu ya kutofautiana kimalengo kati ya Hanscana brand na wanene entertainment. Hanscana alisema ametumia juhudi kubwa sana kuipigania hiyo kampuni kama yake from zero to hero, mpaka kufikia kuwa moja ya kampuni kubwa ya videos hapa Afrika Mashariki.
Hascana alisema kuwa anahitaji kuwa na kampuni yake mwenyewe na hakuna ubaya kati yake na wanene entertainment.
"Kitu ambacho nilikipigania mwenyewe siwezi kukiongelea vibaya, hata kwa bahati mbaya".
Hanscana alimaliza kwa kusema, ameamua kuweka wazi jambo hilo kwasababu amekuwa alipigiwa simu sana na waandishi, bloggers.
Sunday, August 14, 2016
SHILOLE KATIKA PENZI JIPYA.
Keeping up with Diva whatsapp leo paliwaka moto, mapovu yakawatoka watu wengi kutaka kujua nini kinaendelea kati yao, kwasababu picha za Shilole akiwa kwenye pozi la kimahaba na Hamadai zilikuwa zinasambaa instagram.
Mapovu yalikuwa yanawatoka watu kwasababu inasemekana Hamadai ana mpenzi wake. Lakini Keeping up with Diva iliamua kuwapigia hao wahusika kwa kuweka conference call ili kila mtu akifunguka mwenzie asikie.
Hatimaye Hamadai alikiri kuwa yeye na Zahra (mpenzi wake wa zamani) walishaachana siku nyingi kwa sasa yupo na Shilole.
KEVIN HART AFUNGA PINGU ZA MAISHA NA MPENZI WAKE WA SIKU NYINGI ENIKO PARRISH.
Kevin na Eniko wameapa mbele ya mashahidi kuwa watakuwa pamoja kwenye shida na raha huko Montecito, CA kilomita chache kutoka kusini mwa Santa Barbara.
Kev na Eniko walivalishana pete ya uchumba miaka miwili iliyopita lakini inawezekana kuchelewa kwao kufunga ndoa imetokana na wawili hao kuwa na kazi nyingi na kukosa muda.
watu 200 waliohudhuria wameshuhudia motto wa kiume wa Kevin mwenye miaka 8 kuwa msimamizi wa baba yake (best man).
Wasanii wengi walihudhuria ndoa hiyo akiwemo Ludacris.
KYLIE JENNER NA TYGA WAMERUDI LOS ANGELS BAADA YA KUMALIZA MAPUMZIKO YA SIKU YAKE YA KUZALIWA, JE BADO WAPO PAMOJA?
Kylie amewasili kutoka kwenye mapumziko ya kusheherekea siku yake ya kuzaliwa akiambatana na Tyga ambaye inasemekana wamevunja mahusiano yao kwa sasa.
Wawili hao wameshuka kwenye ndege binafsi katika jiji la Angels wakiwa wanatokea Turks na Caicos ambapo walikaa takribani wiki nzima kusheherekea siku yake ya kuzaliwa aliyotimiza miaka 19.
Tyga alishtakiwa na mwenye nyumba wake baada ya kushndwa kuhudhuria kesi yake na kwenda Tropical Island. Lakini Tyga alisuruhisha hilo swala mwishoni mwa wiki iliyopita na akawa huru kuendelea na mambo yake.
Lakini wawili hao walionekana kutokuwa karibu walivyofika Los Angels kama ilivyokuwa imezoeleka.





