Sunday, August 14, 2016

KYLIE JENNER NA TYGA WAMERUDI LOS ANGELS BAADA YA KUMALIZA MAPUMZIKO YA SIKU YAKE YA KUZALIWA, JE BADO WAPO PAMOJA?


Kylie amewasili kutoka kwenye mapumziko ya kusheherekea siku yake ya kuzaliwa akiambatana na Tyga ambaye inasemekana wamevunja mahusiano yao kwa sasa.

Wawili hao wameshuka kwenye ndege binafsi katika jiji la Angels wakiwa wanatokea Turks na Caicos ambapo walikaa takribani wiki nzima kusheherekea siku yake ya kuzaliwa aliyotimiza miaka 19.

Tyga alishtakiwa na mwenye nyumba wake baada ya kushndwa kuhudhuria kesi yake na kwenda Tropical Island. Lakini Tyga alisuruhisha hilo swala mwishoni mwa wiki iliyopita na akawa huru kuendelea na mambo yake.


Lakini wawili hao walionekana kutokuwa karibu walivyofika Los Angels kama ilivyokuwa imezoeleka.

No comments: