Tuesday, August 16, 2016

KUNDI LA ORIGINAL COMEDY LAINGIA MATATANI KWA KUVAA SARE ZA POLISI KWENYE HARUSI YA MASANJA MKANDAMIZAJI.

Katika siku za hizi karibuni, kumejitokeza tabia kwa baadhi ya watu wakiwemo wasanii, watu wengine mmoja mmoja kutumia mavazi yanayofanana na sare za majeshi ya ulinzi na usalama hapa nchini, likiwemo jeshi la polisi katika shuguli zao za kisanii, jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Kwa mujibu wa sheria ya kanuni za makosa ya jinai, sura ya 16 na marejeo yake ya mwaka 2002, kifungu cha 178 (1) na (2)
kinachozungumzia makosa dhidi ya sare za majeshi ya ulinzi na usalama, kinabainisha wazi kuwa ni kosa kisheria kwa mtu yeyote ambaye siyo mtumishi wa majeshi kuvaa mavazi hayo bila kibali kutoka kwa raisi.

Kufuatia kitendo kilichofanywa na kundi la wasanii la Original komedi kuvaa mavazi yanayoshahabiana na sare za jeshi la polisi, jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam linachukua hatua za kisheria juu ya wasanii hao.

Aidha jeshi la polisi linatoa onyo kali kwa mtu ama kikundi chochote kuacha kutumia mavazi yanayofanana na sare zinazovaliwa na majeshi ya ulinzi na usalama hapa nchini na atakayebainika hatutasita kuchukua hatua Kali za kisheria dhidi yake.

Jeshi la polisi linatoa rai kwa wale wote wenye mavazi yanayoshabihiana na sare za majeshi ya ulinzi na usalama kuzisalimisha mara moja katika vituo vya polisi vilivyokaribu nao.

Imetolewa na: Advera John Bulimba- Kamishna Msaidizi wa polisi . (ACP)

Msemaji wa jeshi la polisi
Makao makuu ya polisi.

No comments: