Tuesday, August 16, 2016

MAMA WA KUFIKIA WA RAPPER A$AP AIPONDEA FAMILIA YA KARDARSHIAN.

Kendall Jenner (20) anaweza kuwa matatani kwa kuwa karibu na anayesemekana ni mpenzi wake A$AP Rocky (27), baada ya kusikia mama yake kijana huyo akiongea vibaya kuhusu yeye.

Kari Mayer's ambaye aliolewa na baba yake A$AP kabla hajafariki mwaka 2012, aliongea kwenye interview aliyofanya na Daily Mail kwamba anaamini familia ya Kendall sio nzuri kwa kijana wake.

"kila kitu ninachosikia kuhusu familia hiyo vinanifanya nifikiri kuwa ni familia mbaya  isiyo na maadili kwa Rakim (A$AP) kujihusisha nayo". Alisema mama huyo.

Haieleweki kama Kari ana mahusiano mazuri na kijana wake huyo, kwa sababu alimsema vibaya marehemu mume wake kwenye hiyo hiyo interview, alisema kwamba A$AP anapenda wanawake kama baba yake, kwa sababu baba yake alikuwa na watoto 12 ambao 4 ni mama tofauti.


No comments: