Tuesday, August 16, 2016

WIZKID KUTUMBUIZA KATIKA TAMASHA KUBWA LA FIESTA JIJINI MWANZA.

Msanii wa Nigeria anayetamba na wimbo wake wa Shaba nguli Ayodeji Ibrahim Balogun anayejulikana kwq jina la Wizkid, kutumbuiza katika tamasha la fiesta.

Fiesta ni tamasha linalofanywa kila mwaka, kasoro mwaka jana halikuwepo. Tamasha hilo litafanyika tarehe 20 august Mwanza katika viwanja vya Ccm Kirumba.

Tamasha la fiesta litakuwa linawasanii wengi kutoka bongo flava kama; Mr blue, Rayvan, Baraka da prince, Bilnass, Benpol, Nandy, Young killer, Fid q, Ruby, Madee, Chege, Msami,  Darasa,Jux,Shilole na kwa mara ya kwanza msanii wa visingeli Manifongo kuperfom katika tamasha hilo.

Wizkid ni msanii wa nnje ya Tanzania atakaye perfom katika tamasha hilo.

No comments: