Aliyekuwa mpenzi wa zamani wa IDRIS SULTAN mshindi wa Big brother Africa mwanadada SAMANTHA ame-post kwenye akaunti yake ya instagram picha ya maua aliyopewa na Idris.
Wadau wanadai kuwa hizo ni kiki za Idris lakini zimebuma.
Tazama hiyo picha hapo juu.
Wewe unadhani kweli ni kiki au maneno tu ya mashabiki? Drop comment yako hapa.
Siku ya jana SOULJA BOY alitoa nyimbo yake mpya inayoitwa ''STOP PLAYING WITH ME'' wimbo ambao ulikuwa ni dongo kwa CHRIS BROWN na Chris alipaniki na kuja juu huku akiukandia wimbo huo na kumwambia Soulja boy aache kuimba kama ndo nyimbo zenyewe ndo hizo. Chris alitaka kutoa nyimbo siku ya leo lakini amehairisha kwa sababu leo ni kumbukumbu ya MARTIN LUTHER KING na kuamua kuwa mpole siku ya leo. Unafikiri Chris atatoa nyimbo ya kumjibu Soulja au ataachana na bifu hilo na kuendelea na maisha yake? Drop your comment hapa.
Msanii wa kizazi kipya anayejiita ''SIMBA'' yani DIAMOND PLATNUMZ, jana usiku alifunguka wakati anahojiwa kwenye kipindi cha SPORTS XTRA cha CLOUDS FM.
Diamond alisema anaisapoti Uganda kwa sababu wanaiwakilisha East Africa kwenye michuano hiyo na sababu nyingine ni mashemeji zake kwa ZARI.
Uganda leo usiku wanatupa karata yao ya kwanza kwenye michuano hiyo, wanakipiga vs Ghana majira ya saa 1 usiku kwa saa za Afrika mashariki.