JANUARY MAKAMBA. |
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba leo amezindua Shindano la Kitaifa la Kutafuta Mbadala wa Mkaa ambapo mshindi wa kwanza atashinda kiasi cha Sh 300 milioni.
Amesema madhumuni ya msingi ya shindano hilo ni kuwatambua, kuwatuza, kuwawezesha na kuwaendeleza wabunifu na wajasiriamali wanaojihusisha na mbinu, jitihada za uzalishaji, usambazaji na matumizi ya nishati endelevu za kupikia.
“Natoa wito kwa wadau wote: watu binafsi, wabunifu, kampuni binafsi, wajasiriamali, asasi za kiraia na kijamii, taasisi zisizokuwa za kiserikali, taasisi za elimu ya juu, na taasisi za utafiti, kushiriki katika changamoto hii.”
Amesema moja ya madhumuni ya ziada ya shindano hilo ni kuwaleta pamoja wadau na wabunifu wanaojishughulisha na harakati za kutafuta na kutumia nishati mbadala wa mkaa.
No comments:
Post a Comment