Thursday, November 10, 2016

TIWA SAVAGE MBIONI KURUDIANA NA MUMEWE.

TIWA SAVAGE.
LAGOS, Nigeria
Ikiwa ni takribani miezi sita tangu mwanamuziki mahiri Tiwa Savage atengane na mumewe, Tunji Balogun maarufu kama  Tee Billz, mkali huyo anasemekana kuwa mbioni kurejea katika uhusiano na mumewe huyo wa zamani.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vilivyopo karibu na mwimbaji huyo, kwa jinsi anavyoonekana katika mazungumzo yake kinara huyo yupo tayari kurudiana na mzazi mwenzake huyo.
“Tayari familia zote mbili zimeshakutana kwa ajili ya kufanya majadiliano ya amani,” kilieleza chanzo cha habari.
“Unaweza usiamini maneno yangu lakini maridhiano kati ya Tiwa na Teebillz yapo mbioni. Ameshawaeleza watu wa karibu  kwamba ana mkosa sana Tunji na anataka arejee katika maisha yake. Vilevile wana mtoto wao wa kiume Jamal (Jam Jam) na  pia Tiwa anataka mwanawe akue akiwa karibu na wazazi wake,” kiliongeza chanzo hicho.
Chanzo hicho kilikwenda mbali zaidi kikieleza kuwa mwanamama huyo pia amempa masharti Teebillz kuhakikisha masuala yote ambayo yalianikwa hadharani kisitokee tena.
Mbali na vyazo hivyo, Tiwa vilevile mwenyewe binafsi alisema kuwa alishakutana na mumewe pamoja na washauri ambao walimweleza kuipa nafasi tena ndoa yake na kuheshimu kiapo ambacho alikula madhabauni.

No comments: