1. Barron Trump ndiye mwana wa pekee wa Donald na mke wake wa sasa Melania. Ingawa alijitokeza katika mikutano kadha ya kampeni, mvulana huyu wa miaka 10 hajakuwa akioneshwa sana hadharani. Hucheza gofu na babake na anaaminika kuzungumza Kislovenia kwa ufasaha.
2. Melania Trump, ni mwanamitindo wa zamani, mzaliwa wa Slovenia, ambaye aliolewa na Donald Trump Januari 2005. Alijitokeza na kumtetea mumewe baada ya kanda ya video kutokewa wakati wa kampeni na kumuonesha akijitapa kuhusu kuwadhalilisha kimapenzi wanawake.
3. Jared Kushner ni mume waIvanka, binti mkubwa wa Donald. Bw Kushner ni mwana wa mfanyabiashara tajiri wa New York anayefanya biashara ya nyumba ya ardhi. Amekuwa pia mmiliki wa gazeti la kila wiki la Observer jijini New York kwa miaka 10. Kushner, ambaye ni Myahudi, anadaiwa kuwakera watu wa familia yake alipoandika makala kutetea hatua ya Donald Trump kutumia Star of David (Nyota ya Daudi ambayo ni nembo ya Wayahudi) kwenye ujumbe kwenye Twitter akimshambulia Hillary Clinton. Akiandika kwenye gazeti hilo lake, alisema: "Shemeji yangu hana chuki dhidi ya Wayahudi".
4. Ivanka Trump labda ndiye mwana wa Donald Trump anayefahamika zaidi na watu. Ndiye binti wa pekee wa mke wa kwanza wa Trump, Ivana. Alikuwa mwanamitindo mzamani lakini sasa ni makamu wa rais wa shirika la The Trump Organization na pia jaji katika kipindi cha runinga cha babake cha The Apprentice. Alibadili dini na kujiunga na didi ya Kiyahudi baada ya kuolewa na Jared mwaka 2009.
5. Tiffany Trump ni binti wa Donald Trump kutoka kwa mke wake wa pili Marla Maples, mwigizaji wa zamani na nyota wa TV. Hutumia sana Twitter na Instagram, na ujumbe wake mitandao ya kijamii huashiria maisha ya kifahari.
TIFFANY TRUMP |
6. Vanessa Trump, ambaye jina lake la kuzaliwa ni Haydon, aliolewa na Donald Trump Jr mnamo Novemba 2005. Wawili hao wamejaliwa watoto watano, akiwemo Kai, mwenye umri wa miaka minane (pichani). Vanessa alianza uanamitindo akiwa mtoto na wakati mmoja alikuwa mpenzi wa Leonardo DiCaprio.
7. Kai Trump ndiye kifungua mimba wa Vanessa na Donald Jr, ambao wamejaliwa watoto watano.
8. Donald Trump Jr ndiye mwana wa kwanza wa kiume wa Donald Trump na mke wake wa kwanza Ivana. Kwa sasa ni makamu wa rais mtendaji wa shirika la The Trump Organization. Alimuoa Vanessa Haydon baada ya wawili hao kukutanishwa katika hafla ya maonyesho ya mitindo na babake.
DONALD TRUMP JR |
9. Eric Trump ndiye mwana wa tatu wa Trump na Ivana. Sawa na nduguze, yeye pia ni makamu wa rais mtendaji wa Trump Organization. Yeye pia ni rais wa Trump Winery jimbo la Virginia na husimamia klabu za gofu za Trump.
10. Lara Yunaska, ni mwandaaji vipindi wa zamani katika runinga na hushiriki mashindano ya mbio za farasi. Aliolewa na Eric mwaka 2014. Aliumia vifundo vya mikono yake miwili akipanda farasi wiki mbili kabla ya harusi yake, sherehe iliyoongozwa na Jared Kushner. Wawili hao hawana mtoto, lakini wana mbwa kipenzi.
No comments:
Post a Comment