Polisi nchini Kenya katika jiji kuu Nairobi wamemkamata mlinzi wa Benki ya Equity kuhusiana na wizi mwishoni mwa wiki ambapo wezi walitoweka na mtambo wa kutoa pesa, ATM.
Wezi hao walitoweka na kiasi cha pesa ambacho hakijajulikana kwa sasa wakati wa wizi huo Jumamosi.
Wezi hao walichimba ukuta wa nyuma wa Benki hiyo na kutoweka na sanduku la uhifadhi wa pesa pamoja na mtambo wa ATM, pesa zikiwa ndani.
Washukiwa waliweza kuzima kamera za CCTV na pia kengele ya usalama kabla ya kutekeleza wizi huo.
Akizungumza na BBC, kamanda wa jimbo la Nairobi Japheth Koome amesema kwamba polisi waliweza kupata mitungi ya gesi na vifaa vingine ambavyo hutumuka kukata chuma.
Alipoulizwa kama wezi siku hizi wamepata umaarifa utadhani wanaiga filamu, alisema kwamba kwa siku za hivi karibuni wizi wa benki unazidi kubadilika sana.
Mwaka uliopita, wezi waliojifanya wakaguzi wa hesabu katika benki hiyo walitoweka na dola za Marekani 300,000.
No comments:
Post a Comment