Tuesday, November 8, 2016

KIFO CHA SITTA NI PIGO KWA TIMU YA SIMBA.

ADEN RAGE
Katibu wa Zamani wa Klabu ya Simba, Aden Rage amesema kifo cha Spika wa Bunge mstaafu Samwel Sitta ni pigo kwa wapenzi wa klabu hiyo kwa kuwa ndiye aliyeshiriki kuitunga katiba ya klabu hiyo.
Akizungumza jana (Jumatatu),  Rage amesema huwezi kutaja katiba ya klabu hiyo bila kutaja jina la Sitta.
Rage amesema Sitta wakati wa uhai wake alikuwa mwanachama na mpenzi Mkubwa wa Simba.
Amesema kuna kipindi hata jezi za klabu hiyo zilikuwa zinafuliwa nyumbani kwake.
Amesema Sitta ametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya klabu hiyo ambayo mengine ni vigumu kuyataja.

No comments: