SITTA KUZIKWA JUMAMOSI.
Mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la 9, Samweli Sitta kuwasili nchini siku ya Alhamisi na mazishi ya marehemu kufanyika Jumamosi Urambo, mkoani Tabora.
Siku ya Ijumaa saa 3 asubuhi mwili wa marehemu utaagwa katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar katika ibada itakayoongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa.
Baada ya ibada hiyo, saa 6 kamili mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda Dodoma kwa ndege na saa 8 Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi wengine watauaga kabla ya kusafirishwa kwenda Tabora saa kumi jioni.
No comments:
Post a Comment