MAREHEMU SAID MOHAMED |
Mwenyekiti wa Azam FC, Said Mohamed ‘Mzee Said’ amefariki dunia na anatajiwa kuzikwa leo saa 10:00 jioni kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Azam, Idrissa Nassor amesema Mzee Said amefariki katika Hospitali ya Aga Khan alikolazwa kutokana na kusumbuliwa na shinikizo la damu na ugonjwa wa figo.
“Ni kweli tumepatwa na msiba wa mzee wetu, Mzee Said. Amefariki dunia jioni hii (jana jioni) na alikuwa amelazwa Hospitali ya Aga Khan kutokana na matatizo ya shindikizo la damu na figo,” amesema Nassor.
Nassor ameongeza kuwa swala ya kumuombea marehemu itafanyika katika Msikiti wa Maamur uliopo Upanga kisha kuzikwa kwenye makaburi hayo ya Kisutu.
Enzi za uhai wake, Mzee Said alikuwa ni mmoja wa waanzilishi wa klabu ya Azam FC na mwenyekiti wa klabu hiyo hadi mauti yalipomfika. Pia alikuwa Meneja wa Kampuni ya Said Salim Bakhresa.
No comments:
Post a Comment