MTOTO AKIWA NA MAMA YAKE. |
Mwanamziki wa hiphop Kala Jeremiah leo amepost kwenye akaunti yake ya instagram akielezea jinsi video yake ya WANANDOTO ilivyowakutanisha mama na mtoto ambao walipotezana mwaka jana. Aliandika maneno yafuatayo;
''Siku tatu zilizopita nilipigiwa simu na mtu akaniambia Kuna mama kamuona mtoto wake kwenye video yangu ya wanandoto na mtoto huyo alipotea tokea mwaka Jana mwezi wa 9 mama wa mtoto alifanya jitihada zote za kumpata mtoto wake Bila mafanikio lakini juzi juzi akiwa anatazama video ya WANANDOTO akamuona mwanae kwenye video hiyo Hali iliyompelekea kupata mshangao na mshituko ndipo alipoamua kumtafuta mtangazaji flani wa redio flani ndipo mtangazaji huyo akanitafuta na kuniunganisha na mama huyo. Mama yule alinieleza kwa masikitiko makubwa Sana kuwa mtoto wake alipotea toka mwaka Jana mwezi wa 9 alimtafuta Sana kila sehemu alienda kwa waganga wengi alienda kwenye maombi ya kila aina lakini hakufanikiwa kumpata mwanae mwaka alipokuja kumuona kwenye video ya wanandoto. Baada ya mama huyo kunieleza yote hayo nikawasiliana na kituo cha kulelea watoto cha CHAKUWAMA ambapo mtoto ADAM analelewa nikawaeleza Habari hii wakakili kweli Adam yupo na ni kweli walimpata mwaka Jana mwezi wa 9. basi nikawasiliana Tena na mamayake Adam na kumwambia kuwa nimewasiliana na mlezi wa kituo amekiri kuwepo kwa Adam kituoni hapo na kwakuwa mimi sipo dar kwa Muda huu nikamuunganisha mama Adam na mlezi wa kituo kile wakawasiliana na Jana mama Adam amefika kituoni pale na kuonana na mwanae na amefurahi Sana''.
No comments:
Post a Comment