Tuesday, January 24, 2017

MWANAMITINDO MWENYE JINSIA MBILI.

Mwanamitindo Hanne Gaby Odiele amefichua kwamba alizaliwa na jinsia mbili.
Mwanamitindo Hanne Gaby Odiele amefichua kwamba alizaliwa na jinsia mbili.
Gaby mwenye umri wa miaka 28 anasema kuwa ameamua kutangaza jinsia yake ili kuhamasisha watu kuhusu watu wenye jinsia mbili mbali na kutoa hamasa kwa jamii.
Ni miongoni mwa wanamitindo wa hadhi ya juu kuzungumzia kuhusu jinsia yake.
Watu wenye jinsia mbili hawana viungo vya ndani ama vya nje vinavyowatambulisha moja kwa moja kuwa na jinsia ya kiume ama ile ya kike.
''Nimefikia wakati katika maisha yangu ambapo nimeamua kutangaza jinsia yangu'', alisema Hanne.
''Ni wakati wa watu wenye jinsia mbili kujitokeza, kuondoa uoga na kuzungumzia maswala ambayo yalitukumbuka tukiwa watoto''.
Hanne ameshiriki katika kuuza mitindo ya Chanel na Prada na pia amekuwa katika kampeni za Mulberry na Balenciaga.

WASANII 5 WA KIKE AFRIKA WANAOTENDEA HAKI MASHABIKI ZAO WAKIWA STEJINI WAKITUMBUIZA.

1. YEMI ALADE.
Image result for YEMI ALADE

2. VANESSA MDEE.
Image result for VANESSA MDEE

3. VICTORIA KIMANI.
Image result for VICTORIA KIMANI

4. TIWA SAVAGE.
Image result for TIWA SAVAGE

5. SEYI SHAY.
Image result for SAY SHAY

LIST YA WATANZANIA WALIOINGIA KWENYE TUZO ZA HIPIPO ZA UGANDA.

The Prestigious HiPipo Music Awards |#HMA2017, 4th/Feb/2017 at Serena
WIMBO BORA WA MWAKA TANZANIA.
AIYOLA - HARMONIZE

KAMATIA - NAVY KENZO

AJE - ALIKIBA

SALOME - DIAMOND PLATNUMZ ft RAYVANN

KAJIANDAE - OMMY DIMPOZ ft ALIKIBA

ZIGO REMIX - AY ft DIAMOND PLATNUMZ

SU - YA MOTO BAND ft RUBY

NIROGE - VANESSA MDEE

WIMBO BORA AFRIKA MASHARIKI.
KAMATIA - NAVY KENZO

ZIGO REMIX - AY ft DIAMOND PLATNUMZ

SALOME - DIAMOND PLATNUMZ ft RAYVANN

VIDEO BORA YA MWAKA AFRIKA MASHARIKI.
SALOME - DIAMOND PLATNUMZ ft RAYVANN

JE UTANIPENDA? - DIAMOND PLATNUMZ

MSANII MWENYE VIEWS WENGI YOUTUBE.
Tanzania kaingia DIAMOND PLATNUMZ peke yake.



MPIGIE KURA JIHAN KWENYE MASHINDANO YA MISS UNIVERSE.


"VOTE! VOTE! VOTE!!The door is open
sasa tunaweza kumpigia kura mrembo wetu @jihandimack
Kwakutumia Applications tulizopakua na kama bado hujapakua basi waweza pakua sasa na umpigie kura @jihandimack
kutoka Tanzania.

Jinsi ya kumpigia kura Jihan katika mashindano ya Miss Universe kuanzia tarehe 23 January 2017:


1) VODI: Pakua Vodi app katika Google Store au Apple Store
2) Kupitia tovuti ya www.missuniverse.com
3) MISS U APP: Pakua Miss U app
4) TWITTER: Tweet kwa kutumia hashtag #MissUniverse alafu utatumia hashtag maalum ya Jihan itakayotolewa muda si mrefu. 


Upigaji kura utakapoanza kila mtu ataweza kupiga kura mara 10 kwa siku kwa kila akaunti aliyoisajili.

Kumbuka kuwa website ya missuniverse.com ni mtandao pekee ambapo upigaji kura utaendeshwa

Saturday, January 21, 2017

ALICHOKIANDIA FARAJA NYARANDU INSTAGRAM KUHUSU MELANIA TRUMP.


Mwaka 1996, Melanija Knavs akiwa na miaka 26 aliingia Marekani akiwa na ndoto ya kuwa mwanamitindo. Jana, akiwa ni Melania Trump, alishika Biblia aliyotumia kuapa Rais wa 45 wa Marekani, Rais Donald Trump.


Ukiniuliza kama alidhani kuna siku angesimama Capitol Hill kwenye uapisho wa Rais kama Mke wa Rais wa Marekani, nitakwambia hapana. Lakini ndivyo Mungu alivyo. Leo hii huhitaji kumheshimu Melania Trump, ila utaheshimu mamlaka yake, na kwakuwa amekalia hicho kiti chenye mamlaka, utajikuta unamheshimu tu.


Unaweza kudhihaki historia yake, lafudhi yake au hata kazi aliyokuwa anafanya. Ila Mungu keshampa kibali cha kuwa hapo. Hata huyo Askari ukute alimpigia kura Hillary ila anajikuta akitii mamlaka ya Melania.


Kiongozi anaweza akatoka sehemu chakavu isiyo na tumaini. Chini, mwisho kabisa. Kumbuka hata Bwana Yesu alizaliwa katika zizi la ng'ombe. Mungu anaweza kumuinua mtu usiyemtarajia na kumfanya mtawala wako. 


Mungu anaweza kukuinua wewe usiyejidhania na kukuweka mahali pa juu. Mipango Yake si kama yetu. Usidharau mtu yeyote na muhimu Usijidharau. Njia Zake si kama zetu.

Friday, January 20, 2017

TAMASHA KUBWA LA DIAMOND PLATNUMZ KUFANYIKA UWANJA WA TAIFA.

Image result for SALAAM SK
SALLAM SK.

Meneja wa Diamond Platnumz, fundi mitambo Sallam SK ametangaza ujio mpya wa tamasha kubwa la Diamonds Are Forever 2017 ambapo safari hii litafanyikia katika uwanja wa Taifa.

Muimbaji huyo alifanya tamasha hilo kwa mara ya kwanza nchini mwaka 2012 katika ukumbi wa Mlimani City show ambayo ilihudhuriwa na watu wengi kwa kiingilio cha Tsh 50,000.
.
Sallam alizungumza live na mashabiki katika mtandao wa Instagram (Insta Live) alisema show hiyo ipo kwenye maandalizi na itafanyika uwanja wa Taifa.
.

“Mjiandae na Diamonds Are Forever 2017, Diamonds Are Forever 2017 is back,” alisema

Meneja huyo alidai safari hii tamasha hilo litafanyika uwanja wa taifa ili kuwapa fursa watu wengi zaidi ya kuudhuria.

QUEEN DARLEEN: SIJAWAHI KUTONGOZWA.

Image result for QUEEN DARLEEN
QUEEN DARLEEN.
Msanii kutoka WCB, Queen Darleen amefunguka jana usiku katika kipindi cha Pillow talk kinachorushwa na Times Fm kuwa, hajawahi kutongozwa.

Queen alisema''kusema ukweli mimi sijawahi kutongozwa na mwanaume, kwa asilimia kubwa mimi ndio huwa nawtongoza wanaume.

SHAMSA FORD: WASANII WENGI HAWAOLEWI KWA SABABU WANATAKA WANAUME WENYE HELA.

Image result for SHAMSA FORD
SHAMSA FORD.
Leo katika kipindi cha Leo Tena kinachorushwa na radio stesheni ya Clouds FM, msanii wa kike maarufu kama Shamsa Ford alifunguka na kuhusiana na sanaa yake na mahusiano yake.

Shamsa Ford alisema baada ya ndoa heshima kwa mumewe anayefahamika kwa jina la Chiddy Mapenzi iliongezeka na akaanza kumuogopa, kwa sababu kabla hajaolewa alikuwa anamchukulia poa tu.

Pia Shamsa alisema kuwa wasanii wengi wa kike wa bongo hawaolewi kwa sababu wanataka mwanaume ambaye amekamilika kwa kila kitu, wakati mwanaume anatengenezwa na mwanamke mwenyewe.

Shamsa alimaliza kwa kuwataja wasanii wa bongo movie anaowakubali ni Gabo na Rihama.

WASANII WATAKAO TUMBUIZA KWENYE SHEREHE ZA KUAPISHWA KWA TRUMP SIKU YA LEO.

Jackie Evancho
JACKIE EVANCHO.
Heshima ya kuongoza wimbo wa taifa imepewa msichana wa umri wa miaka 16, Jackie Evancho, ambaye alimaliza wa pili katika shindano la America's Got Talent mwaka 2010.
Sam Moore
SAM NA DAVE.
Sam Moore, wa bendi ya watu wawili ya Sam and Dave, ataongoza wakati wa dansi rasmi ya Liberty and Freedom (Uhuru).
The Rockettes
RADIO CITY ROCKETTES.
Radio City Rockettes pia watatumbuiza katika dansi hizo rasmi, ingawa hatua hiyo ilipingwa na baadhi ya wanachama wa bendi hiyo.
Wengine watakaotumbuiza katika dansi hizo ni Tim Rushlow na bendi yake ya Big Band, Silhouettes, Pelican212, The Piano Guys, Circus 1903, Cache Olson, Lexi Walker na Erin Boheme.
PIA KUTAKUWA NA DANSI ZA WANAOMPINGA TRUMP. Kutakuwa na dansi mbadala - ambazo zinaitwa Dansi za Amani - ambazo zimeandaliwa na wanaharakati watetezi wa uhuru. Miongoni mwa watakaotumbuiza huko ni dadake Beyonce, Solange Knowles.
Solange Knowles
SOLANGE KNOWLES.
Mwanamuziki wa jazz mshindi wa tuzo ya Esperanza Spalding pia atatumbuiza katika Dansi ya Amani mjini Washington.
Esperanza Spalding

KANYE WEST NI RAFIKI TU WA TRUMP LAKINI HATOTUMBUIZA KATIKA KUAPISHWA KWA RAIS HUYO.

Donald Trump na Kanye West
TRUMP NA KANYE WEST.
Kanye West hatatumbuiza wakati wa sherehe ya kuapishwa kwa rais wa 45 wa Marekani, Donald Trump, waandalizi wa sherehe hiyo wamesema.

Kumekuwa na uvumi kwamba tangu nyota huyo wa muziki alipowaambia watu kwamba angempigia Bw Trump kura iwapo angeshiriki uchaguzi, na kisha wakakutana Trump Tower, basi angekuwa mmoja wa wasanii ambao wangetumbuiza Ijumaa.

Lakini Tom Barrack, mwenyekiti wa kamati andalizi ya sherehe ya kuapishwa kwa rais, alisema kwamba sherehe hiyo si "ukumbi ufaao" kwa West.

Alisema mwanamuziki huyo wa mtindo wa rap ni "jamaa mzuri" lakini "hatujamuomba atumbuize."

Bw Barrack alisema: "Yeye hujichukulia kama rafiki wa rais mteule, lakini huu sio ukumbi wake.

"Ukumbi ambao tunao, upande wa watumbuizaji, umejaa, uko sawa, utakuwa kimsingi wa nyimbo za kitamaduni za Marekani, na Kanye ni jamaa mzuri lakini hatujamuomba atumbuize. Tunaendelea na ajenda yetu."

Thursday, January 19, 2017

JENNIFER LOPEZ HAZEEKI BADO ANAONEKANA KIJANA.


Mwanamziki mkongwe na wa siku nyingi J.LO bado anaonekana kijana wakati yupo kwenye miaka ya 40 na kitu huko.

Tazama pichaa yake alivyotupia siku ya jana katika PEOPLE'S CHOICE AWARDS.

NAY WA MITEGO AWATAJA MARAPA 5 ANAOWAKUBALI BONGO.

Nay wa Mitego alikuwa katika kituo cha televisheni cha EAST AFRICA TV katika kipindi cha Planet Bongo na kufunguka marapa 5 anaowakubali hapa bongo:

1. SUGU.
Image result for MR.SUGU

2. FID Q.
Image result for FID Q

3. MR. BLUE.
Image result for MR BLUE

4. MWANA FA.
Related image

5. NAY WA MITEGO MWENYEWE.
Image result for NAY WA MITEGO

WASHINDI WA TUZO ZA PEOPLE'S CHOICE AWARDS 2017.

Image result for people's choice awards 2017
Jana usiku kulitolewa tuzo za People's Choice Awards, wafuatao ni washindi wa Tuzo hizo:

Favorite Animated Movie Voice: Ellen DeGeneres, Finding Dory
Favorite Daytime TV Host: Ellen DeGeneres
Favorite Comedic TV Actor: Jim Parsons
Favorite Dramatic TV Actor: Justin Chambers
Favorite Breakout Artist: Niall Horan
Favorite Cable TV DramaBates Motel
Favorite Cable TV Actor: Freddie Highmore
Favorite Cable TV Actress: Vera Fermiga
Favorite Sci-Fi/Fantasy Actor: Sam Heughan
Favorite Sci-Fi/Fantasy Actress: Caitriona Balfe
Favorite Late Night Talk Show Host: Jimmy Fallon
Favorite Female Artist: Britney Spears
Favorite Female Country Artist: Carrie Underwood
Favorite Country Group: Little Big Town
Favorite R&B Artist: Rihanna
Favorite Pop Artist: Britney Spears
Favorite Social Media Celebrity: Britney Spears
Favorite Animated TV ShowThe Simpsons
Favorite Daytime TV Hosting TeamGood Morning America
Favorite Premium Sci-Fi/Fantasy ShowOutlander
Favorite Network Sci-Fi/Fantasy ShowSupernatural
Favorite Cable Sci-Fi/Fantasy Show: The Walking Dead
Favorite Comedic Collaboration: Britney Spears and Ellen DeGeneres' Mall Mischief
Favorite Social Media Star: Cameron Dallas
Favorite Premium Drama SeriesOrange Is the New Black
Favorite TV Crime Drama Actor: Mark Harmon
Favorite TV Crime DramaCriminal Minds
Favorite Network TV DramaGrey's Anatomy
Favorite YouTube Star: Lilly Singh
Favorite Premium Comedy SeriesFuller House 
Favorite Dramatic Movie Actor: Tom Hanks
Favorite Male Country Artist: Blake Shelton
Favorite Album: Blake Shelton, If I'm Honest
Favorite Dramatic Movie Actress: Blake Lively
Favorite Premium Series Actor: Dwayne "The Rock" Johnson
Favorite Male Artist: Justin Timberlake
Favorite Song: Justin Timberlake, "Can't Stop the Feeling"
Favorite Comedic Movie Actor: Kevin Hart
Favorite TV Crime Drama Actress: Jennifer Lopez
Favorite Humanitarian: Tyler Perry

Favorite Comedic MovieBad Moms
Favorite MovieFinding Dory
Favorite Network TV ComedyThe Big Bang Theory
Favorite Comedy TV Actress: Sofia Vergara
Favorite Thriller MovieThe Girl on the Train
Favorite TV ShowOutlander
Favorite New TV ComedyMan With a Plan
Favorite New TV DramaThis Is Us
Favorite Group: Fifth Harmony
Favorite Action Movie Actor: Robert Downey Jr.
Favorite Actor in a New TV Series: Matt LeBlanc
Favorite Actress in a New TV Series: Kristen Bell
Favorite Competition TV ShowThe Voice
Favorite Hip-Hop Artist: G-Easy
Favorite Dramatic TV Actress: Priyanka Chopra
Favorite Premium Series Actress: Sarah Jessica Parker
Favorite Comedic Movie Actress: Melissa McCarthy
Favorite Cable TV ComedyBaby Daddy



Favorite Movie Icon: Johnny Depp
Favorite Movie Actor: Ryan Reynolds
Favorite Movie Actress: Jennifer Lawrence
Favorite Action MovieDeadpool
Favorite Action Movie Actress: Margot Robbie
Favorite Dramatic MovieMe Before You




Wednesday, January 18, 2017

NAY WA MITEGO: SIJAWAHI KUSIKIA WIMBO MBAYA KULIKO NYIMBO MBAYA NILIZOSIKIA MWAKA HUU KAMA HII.

Siku ya jana Madee (rais wa manzese) na Roma Mkatoriki walitambulisha nyimbo zao kwenye vyombo vya habari na baadae Nay wa mitego alipost huo ujumbe hapo juu kwenye akaunti yake ya instagram bila kumtaja msanii yoyote.

Lakini mashabiki walikomenti kuwa alikuwa anamrenga Madee kuwa ndiye aliyetoa nyimbo mbaya na sio Roma. 

Kwenye mahujiano na kituo cha radio hapa nchini Nay slipopigiwa simu alikataa kuwa hajamrenga Madee ila watu ndio wanasema na sio yeye.

Madee naye alipoulizwa alisema kuwa ameona lakini hawezi kusema kitu kwa sababu hakumtaja mwanamziki huyo au wimbo huo.

Unadhani alichofanya Nay ni sahihi hata kama alikuwa hamrengi Madee? Drop comment yako hapa.

MWANA FA: BILNASS HAKUNIOMBA COLLABO NILIMFANYIA SURPRISE.


Mwana FA amefunguka leo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds Fm wakati wanatambulisha nyimbo mpya aliyoshirikishwa na Bilnass unaoitwa MAZOEA.

Mwana FA alisema ''sikuombwa collabo na Bilnass lakini niliusikiliza wimbo na kwenda kuingiza vocal bila yeye kujua kwa sababu tulikuwa na mipango ya kufanya kolabo, kwahiyo ilikuwa ni surprise kwake kwa sababu mimi na yeye ni marafiki''.

Nenda kwenye link ya Bilnass kusikiliza nyimbo hiyo.

RIDHIWANI: SIHUSIKI NA KUSIMAMIA KAZI ZA BELLE 9.

Kufuatia uvumi ulioko Kitaa kwamba Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh Ridhiwani Kikwete anahusika kumsimamia kazi za Msanii BELLE 9.


Leo kwenye XXL255  ya CLOUDS FM Mh Ridhiwani amefunguka na kusema hivi; Hakuna ukweli wowote mimi kuhusika na kusimamia kazi za Belle 9 nilivutiwa na kazi zake tu.

IDRIS SULTAN AMPA ZAWADI YA MAUA ALIYEKUWA MPENZI WAKE SAMANTHA.


Aliyekuwa mpenzi wa zamani wa IDRIS SULTAN mshindi wa Big brother Africa mwanadada SAMANTHA ame-post kwenye akaunti yake ya instagram picha ya maua aliyopewa na Idris.

Wadau wanadai kuwa hizo ni kiki za Idris lakini zimebuma.
Tazama hiyo picha hapo juu.

Wewe unadhani kweli ni kiki au maneno tu ya mashabiki? Drop comment yako hapa.

Tuesday, January 17, 2017

DIAMOND ASHINDA TUZO ZA TOO XCLUSIVE.


Diamond ali-post kwenye akaunti yake ya instagram kuwashukuru mashabiki zake kwa tuzo hiyo aliyoipata.

RIHANNA AZINDUA PERFUME ZAKE.


Baada ya sandle za Fenty sasa mwanadada machachari kabisa RIHANNA amekuja na perfume inayokwenda kwa jina la KISS BY RIHANNA.

Rihanna kila mwaka anakuja na bidhaa mpya kabisa ambayo inawashangaza walimwengu.

ALICHO-POST BARAKA DA PRINCE INSTAGRAM NA KUFUTA.

Baraka ali-post na kufuta baada ya muda hii post. Hongera Naj mama kijacho.

SOULJA BOY ATOA WIMBO WA KUMTISHIA CHRIS BROWN.

Image result for CHRIS BROWN AND SOULJA BOY
SOULJA BOY NA CHRIS BROWN.
Siku ya jana SOULJA BOY alitoa nyimbo yake mpya inayoitwa ''STOP PLAYING WITH ME'' wimbo ambao ulikuwa ni dongo kwa CHRIS BROWN na Chris alipaniki na kuja juu huku akiukandia wimbo huo na kumwambia Soulja boy aache kuimba kama ndo nyimbo zenyewe ndo hizo.

Chris alitaka kutoa nyimbo siku ya leo lakini amehairisha kwa sababu leo ni kumbukumbu ya MARTIN LUTHER KING na kuamua kuwa mpole siku ya leo.

Unafikiri Chris atatoa nyimbo ya kumjibu Soulja au ataachana na bifu hilo na kuendelea na maisha yake? Drop your comment hapa.

DIAMOND NA ZARI KWENYE JARIDA KUBWA LA AFRIKA KUSINI.


Jarida kubwa na linaloongoza kwa mauzo (PREGNANCY AND BABY GUIDE MAGAZINE) la nchini Afrika ya kusini limempa shavu DIAMOND na mama watoto wake ZARI.


Jarida litatoka wiki ijayo. BIG UP CHIBU.


DIAMOND PLATNUMZ: NAISAPOTI UGANDA KWENYE MASHINDANO YA AFCON KWASABABU NI MASHEMEJI ZANGU KWA ZARI.

Image result for diamond platnumz
DIAMOND & ZARI.
Msanii wa kizazi kipya anayejiita ''SIMBA'' yani DIAMOND PLATNUMZ, jana usiku alifunguka wakati anahojiwa kwenye kipindi cha SPORTS XTRA cha CLOUDS FM.

Diamond alisema anaisapoti Uganda kwa sababu wanaiwakilisha East Africa kwenye michuano hiyo na sababu nyingine ni mashemeji zake kwa ZARI.


Uganda leo usiku wanatupa karata yao ya kwanza kwenye michuano hiyo, wanakipiga vs Ghana majira ya saa 1 usiku kwa saa za Afrika mashariki.



Monday, January 16, 2017

FIFTH HARMONY KUTUMBUIZA KWA MARA YA KWANZA BILA CAMILA CABELLO.

Fifth Harmony, Instagram
FIFTH HARMONY.
Kundi la Fifth Harmony wapo tayari kuwaonyesha mashabiki kuwa wanaweza hata bila ya Camila Cabello ambaye alijitoa mwishoni mwa mwaka jana kwenye kundi hilo.

Kundi hilo litatumbuiza siku ya Jumamosi kwenye 2017 PEOPLE'S CHOICE AWARDS bila ya Camila.

PRIYANKA CHOPRA APATA MAJERAHA WAKATI WA KU-SHOOT SERIES YA QUANTICO.

PRIYANKA CHOPRA.

Priyanka Chopra tweeted, "Thank you for all of your warm thoughts and well wishes. I will be ok, and am looking forward to getting back to work as soon as I can. Much ♥."

Mcheza filamu Priyanka Chopra aliyepata umaarufu kwenye series ya QUANTICO amepata ajari wakati yupo kambini ana-shoot series hiyo.

Alipata majeraha hayo siku ya Alhamisi usiku na kulazwa hospitali. Lakini kwa sasa Priyanka ameruhusiwa kutokana na hali yake kuwa shwari na kuendelea vizuri.

MWANAMIEREKA JIMMY SNUKA AFARIKI DUNIA.

Jimmy Snuka
MAREHEMU, JIMMY SNUKA.
Mwanamiereka wa WWE,Jimmy Snuka maarufu kama 'Superfly' amefariki akiwa na umri wa miaka 73.
Wakili wake amesema mwanamiereka huyo aliaga dunia akiwa katika nyumba ya mkwe wake mjini Florida, akiwa pamoja na familia yake.
Mzaliwa huyo wa Fiji alikuwa wakati mwingi hospitalini kwa shida tofauti ikiwemo ugonjwa wa kiakili wa Dementia, lakini chanzo cha kifo chake bado hakijabainika
Katika taarifa kwenye mtandao wa shirika la WWE imesema imesikitishwa na kifo kilichompata 'mwanzilishi wa kitengo cha high flying' katika ukumbi wamiereka.
Mtoto wake Tamina Snuka, pia nyota wa miereka, aliandika kwenye mtandao wa Twitter, 'Nakupenda babangu' na kuambatisha picha yake na babake kwenye ujumbe wake huo.
Ni chini ya wiki mbili tangu, mashtaka ya mauaji kutupiliwa mbali dhidi yake kuhusiana na kifo cha mpenzi wake mwaka 1983.
Jaji alitoa uamuzi huo baada ya kubaini Jimmy alikuwa na upungufu wa kiakili na hangeweza kuendelea na kesi hiyo ya mauaji ya mpenzi wake Nancy Argentino.
Mashtaka hayo waliwasilishwa mahakamani mwaka 2015.
Alikana madai hayo ya mauaji.
Nyota wa miereka wamekuwa wakituma risala za rambirambi kwa Snuka kwenye mitandao ya kijamii.

Saturday, January 14, 2017

WHATSAPP KUJA NA UWEZO WA KUWAWEZESHA WATUMIAJI KUFUTA UJUMBE KABLA YA KUMFIKIA MUHUSIKA.


WhatsApp-4-840x561

Mtandao maarufu wa kijamii WhatsApp upo katika harakati za kuwawezesha watumiaji wake kufuta ujumbe uliotumwa kabla haujapokewa upande wa pili. 

Kuna wakati unaweza kutuma ujumbe fulani kwa bahati mbaya na kugundua umefanya kosa katika WhatsApp, lakini ukashindwa kuufuta kwa sababu tayari umeshatumwa na kupokewa.
Lakini kwa sasa WhatsApp imekuja na wazo la kurekebisha tukio kama hilo kwenye simu zenye mfumo endeshi wa iOS.

Katika hilo kutakuwa na program katika eneo la ‘Settings’, ambapo utatakiwa kue-‘Edit’ kisha ‘Revoke’ mchakato utakaowezesha kufuta ujumbe huo kwa wakati mara tu unapogundua umekosea.
Hata hivyo, kikubwa ni kuwa utaweza kufanya hivyo kama tu uliomfikia bado hajausoma, ikimaanisha iwapo ameshausoma hutaweza kuufuta.

Lakini hadi sasa WhatsApp hawajatoa taarifa rasmi ya lini uwezo huo utaanza kutumika.

Monday, January 2, 2017

DARASA AFUNGA MWAKA KWA KISHINDO NA MUZIKI.

Tumezoea kusikia nyimbo za mapenzi zikipendwa zaidi kuliko zile zenye ujumbe wa masuala mengine muhimu kwa jamii. Mara nyingi ngoma zenye meseji ni zile zinazohusisha mtindo wa kofokafoka yaani Rap.
Kwenye historia ya Bongo Fleva, nyimbo za Rap hazikuwahi kuzizidi zile za mapenzi. Ngoma zenye jumbe za mapenzi zinapendwa zaidi sokoni na ndiyo  zinazochezwa zaidi.
Sasa inakuwaje pale ambapo rapa anavunja rekodi nyingi kwa wakati mmoja ambazo kwa miaka mingi marapa wengine wameshindwa kuzivunja?
Hapo ndipo Swaggaz linapomkumbuka Ramadhan Sharif  ‘Darassa’ ambaye ni bosi wa Lebo ya Classic Music Group (CMG), ambaye anafunga mwaka kwa historia ya aina yake akiwa na ‘Wimbo wa Taifa’ Muziki.
Mwaka ulipoanza Darassa alitupa karata yake ya kwanza kupitia Kama Utanipenda, aliyomshirikisha Rich Mavoko.
Juni 30, akakutana na waandishi wa habari kutambulisha lebo yake ya CMG, staili yake ya kucheza anayoiita Zombie Walk na kuwaweka tayari mashabiki kwa Too Much, wimbo uliotoka Julai 12.
Grafu ya muziki wa Darassa ilizidi kupanda Novemba 23, alipotambulisha ngoma yake mpya, Muziki. Wimbo unaokua siku baada ya siku – wimbo ulioibua vituko mtaani na kupenya mpaka kwa viongozi wakubwa wa Serikali.
Hii ndiyo ngoma yenye mzunguko mkubwa kwa sasa kwenye redio, runinga mpaka kitaa. Usipousikia kwenye nyumba/chumba cha jirani yako basi utausikia kwenye baa iliyo karibu na wewe.
Ni ngumu kuukwepa labla uwe na matatizo ya usikivu ingawa utauona kwenye runinga hata ukiwa una uono hafifu basi utausikia kwenye Bajaj na bodaboda hapo mtaani.